KATTIBU MKUU KIONGOZI, Phillemon Luhanjo(kulia) alitangaza uamuzi huo katika mkutano wake na waandishi uliofanyika Ikulu, Dar es Salaam juzi akisema Jairo hana hatia na jana anapaswa kurejea kazini mara moja.
Alisema matokeo ya uchunguzi dhidi yake yamebainisha kwamba hakuwa na hatia hivyo kusema kwa mamlaka aliyonayo kwa mujibu wa Sheria namba 8 ya Utumishi wa Umma ya mwaka 2002 na kanuni zake za mwaka 2003, anamrejesha kazini Jairo... “Ninaamuru David Jairo arejee kazini kuanzia siku ya Jumatano (jana).”
KUMBUKA kuwa..... tuhuma hizo zilitolewa na Mbunge wa Kilindi (CCM), Beatrice Shellukindo na hata kumfanya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuzitolea maelezo Bungeni akisema akama angekuwa na mamlaka, angelitolea uamuzi (kumwajibisha mhusika) lakini akaahidi kulifikisha kwa Rais ambaye alisema ndiye mwenye mamlaka ya uteuzi.
Tehe! mwisho wa siku shangwe kama kawaiiiida'
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.