Mchezaji maarufu wa mpira wa Kikapu duniani Dwight Howard akimkabidhi Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete zawadi ya jezi wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam jana.Dwight Howard ni mchezaji nyota wa timu ya kikapu ya Orlando Magic ya nchini Marekani.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete(kulia),Balozi wa Marekani nchini Tanzania Alfonso Lenhardt (kushoto) wakiwa katika picha ya pamoja na nyota wa mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard (Katikati)wakati nyota huyo alipomtembelea Rais ikulu jijini Dar es Salaam jana.Nyota huyo anachezea klabu ya Orlando Magic.
Nyota mchezo wa kikapu nchini Marekani Dwight Howard akimwangalia Simba aliyekaushwa kitaalamu na kupamba lango la ikulu jijini Dar es Salaam huku akifurahia jambo na Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati nyota huyo alipokwenda ikulu kumsalimia Rais na kutoa ahadi ya kutoa msaada ili kukuza vipaji vya mchezo huo nchini. (Picha na Freddy Maro).
Alhamis ya Kitajiri na Meridianbet Imefika
-
NI siku nyingine kabisa ya Alhamisi ambapo leo hii tutaenda kushuhudia Nusu
Fainali za pili za Europa League na Conference huku Meridianbet wakiweka
o...
”Rasmi Soko Kuu la Manispaa ya Bukoba lavunjwa”
-
Soko Kuu la Manispaa Bukoba limevunjwa ili kupisha ujenzi wa soko jipya la
kimataifa unaotarajiwa kuanza muda wowote.
Kwa Wakati tofauti wameonekana Wafa...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.