Masanduku ya kuhifadhia mbogamboga kwaajili ya upangwaji katika madaraja ya ubora husafishwa kwa uangalifu wa hali ya juu toka kwa wakulima wa shamba hili.
Shughuli ya uchambuaji.
Uchumaji Nyanya kwenye shamba hili ni wa manufaa kweli hebu fikiri kwa kipindi cha miezi 6 hadi 8 we unachuma tu nyanya babake! kisha mashina hung'olewa na kupandwa mbegu upya.
Mzigo wenyewe.
Masalia ya makopo ya dawa za kuulia wadudu hutobolewa, tobolewa ili kuepusha wananchi kuyaokota makopo hayo kwa matumizi ya nyumbani, kwani si wote wanaweza kuyasafisha yanavyopaswa kuondoa sumu iliyosalia.
Shamba la matango na uvunaji.
Haya ndiyo matango yanayozalishwa hapa na Arusha Bloom.
Bendera nyekundu (tahadhari) kielelezo kuwa usipige dawa bila maelekezo au kuchuma mazao yanaweza kuwa yamenyunyiziwa dawa.
Kuna baadhi ya mazao ambayo hayachavushwi kwa upepo isipokuwa kupitia wadudu, moja ya mazao hayo ni matango hivyo kutokana na ukubwa wa mashamba haya kuna mizinga mingi ya nyuki ya kutosha maalum iliyojegwa sehemu mbalimbali ndani ya shamba hili kama unavyoona pichani.
Uvunaji maharagwe machanga.
Maharagwe katika daraja.
Shamba la maharagwe na kingo zake kuzuia wadudu washambualiao mazao na kuaharibu ubora.
Chakufurahisha zaidi wageni wataalamu kutoka Misri huja mara kwa mara kuwakutanisha wakulima wakubwa na wadogo kutoa semina ya kilimo bora. Pichani Wakulima wadogo wadogo wakiagana na wataalamu wa kilimo mara baada ya kupewa darasa juu ya namna bora za kilimo cha manufaa ili kufikia malengo ya kuuza mazao kwenye soko la kimataifa kwa kiwango cha juu.
Much Thanks to CCP for facilitating this event and TAHA support on the same, it now the turn of the 17 Participants to use the education gained from this event by training many farmers who are in the industry in order to see that more Tanzania Farmers are awarded Global GAP certificates and be in position to export their produce.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.