ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, January 6, 2012

NDIKILO AFUKUNYUA UPOTOSHAJI ULIOKITHIRI TAARIFA ZA FEDHA MKOANI MWANZA

MKUU wa Mkoa wa Mwanza Evalist Ndikilo amewaagiza wakurungenzi wote mkoani hapa kuwawajibisha kisheria maafisa watendaji wote wa vijiji wanalioshindwa kutoa taarifa za mapato na matumizi katika sehemu zao za kazi. Ndikilo ametoa agizo hilo katika kikao cha kamati cha ushauri mkoa kilichofanyika leo katika ukumbi wa chuo kikuu cha benki kufuati uzembe unaofanywa na watendaji hao wa kutokutoa taarifa kila baada ya miezi mitatu na badala yake wanatoa mwishoni wa mwaka tena kwa viwango hafifu.

Amesema kuwa watendaji wote wanafanya kazi kwa kutokana na sheria zilizowekwa, kwa wale walioshindwa kuwajibika wachukuliwe hatua kulingana na taratibu na sheria.


Dorice Mwanyika Katibu Tawala Jiji la Mwanza akitoa ufafanuzi.

Mbunge wa jimbo la Busega mh. Titus Kamani ni mmoja kati ya waliohudhuria kikao hicho.

Kuhusu majibu yanayotolewa kuwa wananchi hawahudhurii mikutano ya adhara kwa ajili ya kupokea taarifa za mapato na matumizi, mkuu huyo amesema kuwa hizo sio hoja ya msingi na kama wananchi wameshindwa kuhudhuria vikao hivyo ni wazi kuwa watendaji hao wameshindwa kutawala.

Aidha Ndikilo ametoa onyo kwa watendaji wote kuanzia leo kubandika taarifa hizo kwenye vibao vya matangazo na ameahidi kufanya ukaguzi wa taarifa hizo kwa vijiji vyote kupitia ziara yake anayotegemea kuifanya hivi karibuni.

Wakuu kutoka idara mbalimbali kikaoni.

Pia mkuu huyo amewaonya na kuahidi kuwachukulia hatua watu binafsi, vikundi, wanasiasa na wale wote watakaokwamisha zoezi hilo pamoja na ukusanyaji michango muhimu ya maendeleo kwa sababu zao binafsi.

Joyce Masunga Katibu mpya wa CCM Mkoa wa Mwanza aliyechukuwa nafasi ya Alhaji Mwangi Rajab Kundya aliyehamishiwa jimbo la Mjini Magharibi.

Wajumbe wa kikao.

Kwa ujumla ya halmashauri nyingi za mkoa wa Mwanza zimeshindwa kuwasilisha taarifa zake za mapato na matumizi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.