ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, April 4, 2013

WASANII WA FILAMU MWANZA WATEMBELEA SHULE YA WATOTO WENYE ULEMAVU YA MITINDO

Wasanii wa uigizaji filamu pamoja na uchekeshaji mkoani Mwanza, Mwishoni mwa wiki katika kusherehekea sikukuu ya Pasaka waliamua kufunga safari kwenda katika shule ya watoto wenye ulemavu ya Mitindo iliyoko wilayani Misungwi mkoani Mwanza na kutoa zawadi mblimbali walizokuwa nazo kupitia changizo walilofanya wao kwa wao.

Mwenyekiti wa Umoja wa wasanii wa Filamu Mwanza ujulikanao kama Meet Club akikabidhi kwa mkuu wa kituo kiasi walichochangishana.


Wasanii hao waliimba nao pamoja nyimbo mbalimbali na kila mmoja alishiriki kuwa karibu nao kama mzazi.

Umoja wa wasanii hawa uliiteua siku hiyo muhimu ya Pasaka kudhuru kituo hicho kwa nia ya kuwatembelea watoto hao na kujionea changamoto wanazokutana nazo, kuwafariji kwa kucheza nao na  kufurahi nao hasa ukizingatia ni siku ya sikukuu, 

Hakika watoto walijisikia vyema kutembelewa huku nao wasanii wakijifunza mengi kutoka kwa watoto hawa wanaohitaji roho ya wengi wenye huruma.

Msanii ajulikanaye kwa jina la 'Chenga Mbili' akiwa na watoto wake wa pasaka.

"Hawa ndiyo wanangu na ndiyo rafiki zangu" alisema dada huyu.

Nao watoto walijihisi kupendwa kwa ukaribu ulioonyeshwa na wasanii waigizaji wa jijini Mwanza.

Furaha tele kwani si kukaa nao tu bali watoto hao walishuhudia vimbwanga vya uigizaji.

"Tuwapende watoto hawa kwani wanastahili kupendwa" Ndivyo isemavyo picha hii.

Japo moja ya wawakilishi wasanii na watoto.

Kisha baadaye kabisa msafara wa wasanii hao wa uigizaji filamu na uchekeshaji ulirejea jijini Mwanza huku kila msanii akiwa na wazo lake kichwani kuhusu watoto hao wa Shule ya Mitindo wilayani Misungwi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.