ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 14, 2011

POLISI WASAKA MADAKTARI WALIOTEKWA KENYA

Polisi wakitumia helikopta na magari wanawasaka watu watu wenye silaha waliowateka nyara madaktari wawili wa Uhispania wanaofanya kazi na shirika la misaada la Medicins Sans Frontiers (MSF) karibu na mpaka na Somalia nchini Kenya.

Wawili hao walitekwa katika kambi ya wakimbizi ya Daadab, ambayo inawahifadhi maelfu ya wakimbizi wanaokimbia njaa katika Pembe ya Afrika.

Taarifa zinazohusianasomalia, kenya, ulayaDereva wao, raia wa Kenya, alijeruhiwa na sasa amepelekwa hospitali, limesema shirika la MSF.


Katika wiki za hivi karibuni, wanawake wawili, mmoja raia wa Uingereza na mwingine Mfaransa walitekwa karibu na mpaka huo.

Mwandishi wa BBC Bashkash Jugsodaay akiwa kaskazini mwa Kenya anasema mikakati kabambe inafanywa kuwa saka watekaji nyara hao.

"Asubuhi ya leo wafanyakazi wa MSF walipatwa na tatizo huko Daadab"
MSF imethibitisha kupotea kwa madaktari wake raia wa Ulaya wawili, na wametoa taafifa fupi.


Chanzo: bbc swahili.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.