NA ALBERT G. SENGO/MWANZA
Miongoni mwa vitu ambavyo jamii yetu haijajua, haijakubali au pengine haina huo uelewa wa kutosha kuhusu suala la utalii ni kwamba utalii siyo kufanya ziara mbugani au kutembelea sehemu zenye vivutio vya kale, dhana ya utalii ni kubwa na inazama ikishirikisha masuala mengi sana ndani ya jamii na yanayoizunguka jamii ikiwemo utamaduni, ngoma, majengo mapya, miundombinu ya usafiri na usafirishaji yakiwemo madaraja mapya, maziwa na bahari. Vilevile dhana ya utalii inaingia hadi kwenye mavazi ya asili, viunga vya burudani aka bata na hata mito na milima inayopatikana mahali flani, ambapo safari hii Mtembezi Marathon inakuja kuvumbua na kuainisha maeneo mapya ya utalii Kkatika jiji la miamba (Rock City) Mtembezi Marathon tayari imeshafanyika katika mikoa ya Dar es salaam, Kigoma, Tabora na Dodoma na sasa inaenda kufanyika mkoani Mwanza. #mwanza #samiasuluhuhassan #royaltour #tanzaniaTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.