Waziri Jafo amekemea tabia hiyo inayoendelea kisiwani humo kwasasa baada ya watu wengi kufiwa na wenza wao kutokana na ajali ya kivuko cha MV. Nyerere kilichozama miezi michache iliyopita na kupoteza watu wengi.
Katika ziara yake maalum ya utekelezaji wa agizo la Rais Dk. John Magufuli la ujenzi wa majengo yenye hadhi ya hospitali katika eneo la Ukara, Waziri Jafo amesema zoezi hilo limeanza rasmi leo na kuagiza ujenzi huo ukamilike ndani ya miezi mitatu.
Amesema amepata taarifa kwamba wafiwa wanafanya mapenzi na watu wengine ili watolewe mikosi kitendo ambacho ametahadharisha kwamba kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo kutokana na watu wao kuambukizwa nagonjwa yakiwepo gonjwa la UKIMWI na Ugonjwa wa Ini yaani Hepatitis B.
Jafo amewataka wale ambao bado hawajafanya kitendo hicho cha kutakaswa wasijaribu kabisa kwani kinaweza kusababisha maafa makubwa kisiwani humo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.