Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga,akizungumza na Waandishi wa Habari juu kiasi cha shilingi Bilioni mbili zilizotolewa katika awamu ya kwanza |
Akizungumza na waandishi wa habari leo Novemba 17, Waziri wa Kilimo, Japhet Hasunga, amesema TADB imeanza kulipa wakulima wote walioakikiwa katika mikoa tajwa kupitia vyama vyao vya Msingi na ushirika kwa kuhakikisha fedha hizo zinawafikia wakulima moja kwa moja kupitia akaunti zao.
“Zoezi la ulipaji limeanza jana na kwasasa tumewafikia wakulima zaidi ya 2168 kutoka mikoa mitatu tulionza nayo hivyo tunategemea kuendelea kulipa mpaka kufikia jumatatu tutakuwa tushalipwa wakulima wengi sana kama ilivyoagizwa na Rais Dk . John Pombe Magufuli kutaka fedha hizo ziende kwa wakulima moja kwa moja bila ya makato,”amesema Waziri Hasunga.
Katika hatua nyingine Waziri wa Kilimo ametangaza kuwa jumla ya Tani 20 za korosho zimekamatwa kutoka ghala la mtu binafsi la Olam lililoko mkoani Mtwara ambapo zilikuwa zinahamishwa kwenda kwenye eneo la ununuzi wakati zikiwa ni za mwaka jana.
Amesema korosho hizo zilikabidhiwa katika Chama cha Msingi cha Mnyawi kwa lengo la kuchanganywa kinyemela na zile zinazopelekwa kwenye maghala makuu.
“Jana (juzi) tulikamata tani 20 zilizokuwa zimepenyezwa katika vyama vya msingi, tusingependa lijirudie hivyo, wananchi wawe makini kuhakikisha korosho zinazoletwa katika vyama vya msingi ni zile za Watanzania ili korosho yetu peke yake iendelee kununuliwa na Serikali,” amesema Hasunga.
Amesema korosho zitakazokamatwa kutoka nje au kuingizwa kinyemela kwenye vyama vya msingi zitataifishwa na wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.
Jumanne wiki hii tani nyingine tisa zilikamatwa katika eneo la Newala baada ya kuingizwa kinyemela toka nchini Msumbiji.
Aidha juzi pia yalikamatwa magunia 152 ya korosho katika Wilaya ya Nanyumbu yaliyoingizwa nchini kutoka Msumbiji.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.