ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 13, 2018

VIDEO:- HUU NDIYO MRADI WA MAJI UTAKAO TATUA TATIZO LA MAJI MISUNGWI.



GSENGOtV/MISUNGWI

HEBU vuta kumbukumbu hadi mwaka 2015 aliyekuwa mgombea mwenza wa urais, sasa Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan alizunguka nchi nzima kuendesha kampeni ya kuingia akiangia ikulu akitumia kaulimbiu ya ‘Kumtua mama ndoo kichwani’ akiahidi Serikali ya chama hicho ingemaliza kero hiyo endapo ingeichaguliwa.

Kama haitoshi, aliyekuwa mgombea urais ambaye baadaye aliibuka kidedea, John Magufuli mbali na kampeni, alipoingia madarakani alitamka bungeni akiahidi kuwatua akina mama ndoo vichwani.

Ikiwa ni miaka mitatu sasa kwa Rais John Pombe Magufuli kuwa madarakani hayawi hayawi ndoto hiyo sasa inakwenda kutimia, kwani hapa Mhe.Mongella anakagua chanzo cha mradi wa maji Nyahiti-Misungwi ambao hadi kukamilika kwake mwakani, utaondoa adha ya uhaba wa maji safi na salama kwa wakazi wa Wilaya Misungwi.

Mkuu wa Mkoa Mwanza, Mhe. John Mongella ambaye leo ameanza ziara ya siku mbili wilayani hapa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo afya, maji na elimu, inayo tekelezwa na fedha za Serikali ya awamu ya 5, amesimamia hatua kwa hatua ikiwa ni sanjari na kuwaweka kitimoto wakandarasi na wasimamizi pale alipokuwa akipatilia shaka kwenye miradi husika.

Mradi wa Maji na Usafi wa Mazingira Misungwi unatekelezwa na kampuni ya China Civil Engineering Construction Corporation (CCECC) kwa gharama ya shilingi bilioni tisa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.