GSENGOtV
Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh Jerry Muro AMEFANIKIWA kupata msaada wa mbuzi mia moja ( 100) wa Kisasa wa maziwa kutoka IRELAND 🇮🇪 kwa ajili ya kinamama Jane wanaotoka katika kaya Maskini wilayani humo ambao ni Msaada kutoka kwa Mkurugenzi wa Kituo cha Teknolojia za kilimo na ufugaji ECHO Ndugu Erwin Kinsey ambaye ameshirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kutoka nchini Ireland.
Dc Muro ambae ameazimia kuwakomboa kina kama Kwa kuwatafutia misaada mbalimbali ya kujikombe amewataka wakinamama hao kutumia msaada huo kuwa kama mbegu katika kujiendeleza katika jamii zao na kuowaongezea kipato waweze kuendesha Familia zao na kutoa Ombi Kwa kina mama hao kutothubutu kuwauza mbuzi hao wala kuwafanyia matumizi mengine tofauti na ufugaji ili waweze kutimiza malengo yaliyokusudiwa Kutokana na msaada huo
Pia Mhe. Muro amemshukuru Mkuu wa Jimbo la Arusha Magharibi dayosisiya Kaskazini kati ya Kanisa la kuingilia la Kilutheri Tanzania KKKT Mchungaji Philemon Mollel * kwa kushirikiana na Ndg. *Erwin Kinsey wa Kituo cha ECO Katika kuongeza jitihada zake kwa kushirikiana na serikali kupitia shirika la Tasaf kusaidia kaya masikini kwa kuwaletea mbuzi hao ambao watawasaidia baadhi ya kina mama hao kuleta maendeleo katika Wilaya ya Arumeru.
Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.