NA VICTOR MASANGU,BAGAMOYO
Wafugaji wakiwemo baadhi ya wafanyabiashara katika soko la mnada wa mifugo uliopo lata ya Zinga wameiomba serikali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha inawajengea miundombinu ya machinjio ya kisasa pamoja na choo kwa lengo la kuweza kupata eneo lenye ubora na mazingira mazuri ya kufanyia kazi.
Baadhi ya wafanyabiashara hao wakizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti katika eneo hilo la Zinga kwamtoro wamesema kwamba kwa kwa sasa eneo ambalo wanalitumia kwa ajili yakuchinjia mazingira yake ni mabaya na haliko katika ubora mazuri hivyo kunaitajika uboreshaji wa machinjio na pamoja na miundombinu ya vyoo.
Mmoja wa wafanyabiashara katika eneo hilo Idd Omari amesema kwamba soko hilo ni sehemu ya kukuza uchumi kwa wakazi wa Zinga na Bagamoyo hivyo ni vema Serikali ikaona umuhimu wa kujenga miundombinu imara ya machinjio na zizi la Mifugo.
"Awali tulikuwa tunauza mbuzi watatu hadi wa nne siku ya mnada ila kwasasa ni kuanzia mbuzi kumi hii ni sehemu yetu ya biashara inayokuza uchumi wetu tunachoomba ni kujengewa miundombinu imara Ili tufanye biashara zetu vizuri," alisema Omari.
Akizungumzia suala la kukosekana kwa Zizi Omari alisema wapo wafugaji wanaleta mifugo yao mingi lakini hawana sehemu ya kuihifadhia hivyo endapo kutakuwa na zizi itawasaidia kubeba Mifugo mingi zaidi.
Naye Suzana Kazimoto alisema kuanzishwa kwa soko hilo la mnada katika eneo la Zinga kinakwenda kuinua uchumi wa wafanyabiashara na Wanawake wajasiriamali katika eneo hilo.
Muro Shakaire mfanyabiashara katika soko hilo aliishukuru Serikali kwa kuanzisha mnada huo ambapo alisema Ili wafanye kazi vizuri Halmashauri ijenge miundombinu imara ikiwemo machinjio Bora.
Kutokana na kikwazo kingine cha maji katika soko la mnada huo Kampuni ya EGCORE inayojishughulisha na mambo ya kijamii imeahidi kuchimba visima kukabiliana na tatizo hilo
Kaimu Mkurugenzi wa Kampuni hiyo Yusuph Mjema alisema wanatarajia kutumia sh. Miln 28 kwa ajili ya kuchimba visima hivyo kwenye kila kibanda katika soko hilo kuweze kupata huduma ya maji karibu.
Mjema alisema uwepo wa visima hivyo hautazuia jitihada za Serikali kuunganisha miundombinu ya maji katika soko hilo na kwamba maji yatokanayo na visima hivyo pia mbali ya kutumia na wafanyabiashara wananchi waishio karibu na soko la mnada huo watanufaika nayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.