NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
TAKUKURU MKOA WA MWANZA YATOA ELIMU Kwa kipindi cha mwezi Julai hadi Septemba kuelekea kipindi cha Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka huu,Takukuru Mkoa wa Mwanza imetoa elimu ya dhana na madhara ya Rushwa kwenye uchaguzi, makatazo dhidi ya rushwa na wajibu wa wananchi kushiriki kuzuia vitendo vya rushwa kabla,wakati na baada ya uchaguzi ikiwemo na kutoa taarifa za vitendo vya rushwa. Takukuru Mkoa wa Mwanza kupitia kazi ya Uchambuzi wa mfumo kuhusu mapato yatokanayo na mauzo ya mifugo katika mnada wa Misasi Wilayani Misungwi imewezesha kuongezeka kwa mapato kutoka wastani wa shilingi milioni 2 laki 5 hadi milioni tatu mpaka kufikia milioni saba hadi milioni nane kwa mnada mmoja ambalo ni ongezeko la zaidi ya asilimia 100Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.