ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 19, 2024

HIZI NDIZO SABABU ZA KAMPUNI YA HUDUMA ZA MELI KUBADILI JINA NA KUWA TASHICO

Na ALBERT G.SENGO, MWANZA.


NAIBU waziri wa Wizira ya Uchukizi David Kihenzile, amezindua jina jipya na nembo ya Kampuni ya Meli Tanzania,kutoka Kampuni ya Huduma ya Meli na kuitwa Kampuni ya Meli Tanzani,(TASHICO) au Tanzania Shipping Company.

Akizungumza kwa niaba ya Waziri wa Uchukuzi, Makame Mbarawa,katika hafla fupi ya uzinduzi huo, Kihenzile, amesema hatua ya kubadilisha jina ni mhimu sana katika kuimarisha miundombinu ya kusafirisha shehena za mizigo, hivyo TASHICO inapaswa kuweka mipango thabiti ya kuendelea kuimarika.

Amesema kuna baadhi ya watendaji wanapewa dhamana ya kusimamia miradi, lakini wanaharibu fedha na kuleta miundombinu haina viwango, hivyo TASHICO, fedha wanazokusanya wahakikishe zinatumika kwa utaratibu na kuongeza mkakati wa masoko, huku akiwataka mpango wa kuongeza Meli Bahari ya Hindi ufanyike haraka maana wateja wanusubiri kwa hamu safari hizo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.