ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 25, 2016

RIDHIWANI,DIWANI WA VIGWAZA WAGOMEA KUPOKEA MRADI WA MAJI CHALINZE.

NA VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
 
MBUNGE wa jimbo la Chalinze,Ridhiwani Kikwete ameungana na wakazi wa vijiji vitatu vya Kidogozelo,Kitonga na Milo,kata ya Vigwaza ,kukataa kukabidhiwa mradi wa maji uliogharimu kiasi cha sh.Mil 258 fedha kutoka bank ya dunia 
 
Mradi huo umekataliwa kutokana na kutokamilika pamoja na kuonekana mapungufu makubwa ikiwa ni pamoja na mabomba kuwekwa karibu na ardhi,kupasuka kabla ya matumizi na kutandazwa mabomba madogo yasiyokdhi mahitaji.
 
Kutokana na kasoro hizo kubainika Ridhiwani ametoa mwezi mmoja kwa idara ya maji halmashuari ya wilaya ya Bagamoyo kuhakikisha inafanya marekebisho na ukaguzi wa kina .
 
Hayo yamejiri baada ya wataalamu kutoka halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo ambao waliambatana na wahandisi kutoka wizara ya maji kumuita mbunge huyo kwa malengo ya makabidhiano ya mradi katika vijiji hivyo.
 
Ridhiwani amewataka wakandarasi,watalaamu na mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo,Juliana Msagala kuacha masihala kwenye miradi mikubwa inayogharimu kiasi kikubwa cha fedha kutoka serikali na kwa wahisani .

Awali Diwani wa kata ya Vigwaza ,Muhsin Baruhan amesema kutokana na mradi huo kusuasua kunasababisha wakazi wa kijiji hicho kutumia maji ya madimbwi na mtoni hivyo kuhofia milipuko ya magonjwa na kuliwa na mamba.
 
Mhandisi wa idara ya maji katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, Juliana Msagala amekiri kuwepo kwa mapungufu yaliyoonekana na kumuahidi mbunge wa Chalinze Ridhiwani kuwa maagizo aliyoyatoa watayafanyia kazi .
 
Mradi huo ulianza mwaka 1997 na baadae uliingizwa kwenye mpango wa uboreshaji wa mradi katika program ya maji usafi na mazingira vijijini ambapo halmashauri iliingia mkataba na mkandarasi Sajo Engineering Contractor kwa ghamara ya sh mil.258.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.