ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, February 25, 2016

RED CROSS TANZANIA CHATOA MSADDA KWA WAHANGA WA MAFURIKO WILAYANI RUFIJI

NA VICTOR MASANGU,  RUFIJI  PWANI

CHAMA cha Msalaba mwekundu Tanzania  (Red Cross) kimetoa msaada wa mablanketi 300 ya kujifunikia, neti 300 pamoja na ndoo 300 vyenye thamani ya kiasi cha shilingi milioni 10 kwa wananchi waliokumbwa na  maafa  ya  mafuriko  baada ya mvua kumbwa kunyesha  katika  Wilaya ya Rufiji Mkoani Pwani.

Wahanga hao wa mafuriko wamepatiwa msaada huo kutokana na baadhi yao kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu sana kutokana na kutokuwa na makazi maalumu ya kuishi kwani nyumba zao zimezingilwa na maji  pamoja na mazao yao  ambayo walikuwa wanayategemea kwa ajili ya chakula kusombwa na maji.

Akikabidhi msaada huo kwa Mkuu wa Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu katika kijiji cha Utete  Meneja mkuu wa Red Cross Tanzania kutoka kitengo cha kusaidia  maafa   Lenatusi Mkaluka  amesema kwamba wameamua kwenda kutoa msaada   kwa wananchi  hao kutokana na kukumbwa na mafuriko makubwa ambayo yamepelekea  kutokea kwa uharibifu mkubwa wa mali zao pamoja na mazao kusombwa na maji.

Lenatusi alisema  kwamba red cross imeamua kuungana na serikali katika kuwasaidia  msaada huo ambapo kwa upande wao wametoa neti,mablanketi 300 pamoja na ndoo 300 kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao wa wilaya ya rufiji ambao kwa sasa wanaishi katika mazingira magumu.

Kwa upande wake Mkuu wa  Wilaya ya Rufiji Nurdin Babu  mara baada ya kupokea msaada huo amewataka   viongozi na watendaji  kuachana na tabia ya wizi wa  chakula kilichotolewa na serikali pamoja na msaada uliotolewa na  Red Cross  kwa ajili ya wananchi waliokumbwa na maafa ya mafuriko kwa maslahi yao yao binasfi na badala yake wahakikishe msaada huo unawafikia walengwa wenywe bila ya kufanya hujuma ya aina  yoyote ile.

Babu alibainisha kwamba kwa sasa katika Wilaya yake ya Rufiji wananchi  waliokumbwa na mafuriko wanaishi katika wakati mgumu kutokana na kukabiliwa na janga la njaa pamoja na kukosa makazi  licha ya serikai kutoa msaada wa  chakula hivyo viongozi wanapaswa kutokuwa na tamaa wakati wa zoezi zima la ugawaji wa  chakula na sio kupeleka majumbani kwao na kuwaacha wahanga hao kushinda na njaa.

Kwa upande wake Mbunge wa Jimbo la  Rufiji Mohamed Mchengerwa alisema kwamba katika jimbo lake kata zipatazo 12 kati ya 13 zimekumbwa na maafa ya mafuriko na kuongeza kwamba kwa sasa tayari serikali imeshapeleka tani 100 za mahindi  kwa ajili ya kuwasaidia wahanga hao.

Mchengerwa alibainisha kwamba  licha ya serikali kutoa msaada huo wa chakula lakini bado kunahitajika chakula kingine ii kuweza kukidhi mahitaji ya walengwa kwani kilichopo hakiwezi kutumika kwa mudu mrefu kutokana na mahitaji kuwa ni makubwa na kuongeza kuwa anatoa wito kwa wadau na taasisi nyingine kujitolea katika kusaidia misaada yoyote kwa ajili ya wananchi hao.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibiti Ally Ungando alitoa pongezi kwa uongozi wa chama cha msalaba mwekundu Tanzania kwa kutoa msaada huo,kwani madhara yaliyojitokeza kwa wananchi wa rufiji ni makubwa kwani mazao waliyoyapanda kwa ajili ya chakula yote yamesombwa na maji pamoja na wengine kukosa makazi ya kuishi hivyo kunahitajika msaada zaidi kwa wahanga hao wa mafuriko.

 Afisa Kilimo wa Wilaya ya Rufiji Bondesi Mwalibalinga alisema kwamba kutokana   na maafa hayo alitoa wito kwa wakulima wote ambao wanalima katika mabonde kuondoka mara moja kwani mvua bado zinaendeea kunyesha na kubainisha kwamba jitihada ambazo tayari wameshazifanya kukufanya tathmini ya watu waliokumbwa na mafuriko hayo ili kuweza kujua ni namna gani ya kuweza kuwasaidia kwa hali na mali.

WAHANGA zaidi ya elfu 60 wa mafuriko katika Wilaya ya Rufiji Mkoa wa Pwani kwa sasa wanahitaji msaada wa chakula wa tani zaidi ya 1300 ili kuweza kukidhi mahitaji yao,ambao hadi sasa serikali tayari imeshapeleka msaada wa tani 200 za mahindi,ambazo bado hazitoshi hivyo kunahitajika juhudi za makusudi kwa wadau na taasisi nyingine binafsi  kwa ajili ya kuwasaidia wananchi hao.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.