GSENGOtV
Wakati takwimu za kitaifa, zikionesha kuwa zaidi ya Watanzania milioni 1.4 wanaishi na VVU huku mikoa inayoongoza na asilimia yake kwenye mabano ikiwa ni Njombe (11.4), Iringa (11.3), Mbeya (9.3) na Mwanza kwa asilimia 7.2.
Katika takwimu za mkoa wa Mwanza kufikia lengo la Tisini tatu (90,90,90) zinaonyesha kwa 90 ya kwanza ni asilimia 53 tu ya WAVIU wanafahamu hali zao, huku idadi kubwa iliyobaki hawajui hali zao za maambukizi hivyo hawajaanza kutumia dawa za kufubaza VVU.
Mbele ya waandishi wa habari Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ameyatanabaisha hayo hii leo akiongeza kuwa kwa 90 ya pili, waliopimwa na kugundulika kuwa na VVU na kuanza kutumia dawa ni asilimia 74, na takwimu zinaonyesha kuwa wanawake wapo wengi kuliko wanaume. Kwa 90 ya tatu, takwimu za mkoa zinaonesha kuwa ni asilimia 72 tu ya walioanza kutumia dawa na kuwa na ufuasi mzuri wa dawa na wamefanikiwa kufubaza virusi ambao hata hivyo idadi kubwa ni wanawake ndiyo wanaotimiza masharti.
Habari tukioni. |
Kampeni hii ina dhamira ya kutoa taarifa, kuelimisha na kuisaidia jamii kupima virusi vya ukimwi na kutoa matibabu yanayorefusha maisha iwapo watagundulika kuwa na maambukizi ya VVU. |
Mkoa wa Mwanza umepokea agizo la Mheshimiwa Waziri Mkuu ambapo uzinduzi rasmi wa Kampeni utafanyika Jumamosi ya tarehe 21 July 2018 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.