GSENGOtV/-/MWANZA.
Mwezi mmoja baada ya Waziri Mkuu
Kassim Majaliwa kuzindua kampeni ya “Furaha yangu, Pima, Jitambue, Ishi’ jijini
Dodoma kwa ngazi ya kitaifa sasa kampeni hiyo inazinduliwa hapa ikiwa ni Julai
21 katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza kwa ngazi ya mkoa.
Zaidi ya matarajio, viongozi na
wananchi wake kwa waume hata watoto wamejitokeza kwa wingi ili kupima na
kutambua afya zao.
Mabanda ya kupima maradhi mbalimbali
yamesimikwa katika viwanja hivi ambapo ni fursa sasa kwa mgeni rasmi ambaye ni
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella kuyatembelea mabanda hayo kujionea
shughuli za afya na elimu zinazofanyika hata ikibidi naye kupima afya.
Hizi ni Dawa mpya zenye uwezo wa kufubaza
na kukinga maambukizi dhidi ya VVU kwa asilimia 99 zilizoanza kutumika katika
baadhi ya nchi za Kusini mwa Afrika, na sasa zimekuja ukanda huu wa Afrika
Mashariki ndani ya Tanzania. Badala ya kumeza vidonge vingi sasa muathirika
atapaswa kumeza tembe moja tu kujikinga na maambukizi.
Naam mara baada ya kupata elimu ya
kutosha Mhe. Mongella hakusita kupima afya ambapo majibu yalitoka papo hapo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa kampeni hiyo, Mratibu wa
Ukimwi Mkoa wa Mwanza Dk Pius Masele amesema maambukizi ya virusi vya ukimwi
yameongezeka na kufikia asilimia 7.2 kutoka asilimia 4.2, mwaka 2011
Kwa mujibu Dk Masele amesema
ongezeko hilo linaufanya mkoa huo kuwa wanne ukitanguliwa na Njombe,Iringa na
Mbeya.
Kwa upande
wake Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongela, amewataka watendaji wa idara za afya
katika wilaya zote za mkoa huo kuhakikisha wanaandaa mpango kazi utakaoainisha jinsi
watakavyo tekeleza kampeni hiyo ili iwe na tija.
Kampeni
ya furaha yangu inafadhiliwa na serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Shirika la Maendeleo la Kimataifa la Marekani
(USAID) Tanzania kupitia mradi wake wa FHI360- Tulonge Afya wa miaka mitano, Tume ya Kudhibiti
Ukimwi Tanzania(TACAIDS) na Shirika la Kazi
Duniani (ILO) kupitia kipengele cha kusaidia wanaume wenye umri wa zaidi ya
miaka 45 kwa kipindi cha miezi sita .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.