ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 2, 2023

JINA KIBU DENIS LAIBUKA WAKATI SEKILOJO AKIICHAMBUA YANGA YA ZAMA ZAKE NA YA SASA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Alikuwa kiungo mshambuliaji mwenye akili nyingi na sifa ya kutoa pasi maridadi zilizozaa magoli, akinyumbulika dimbani akiwa na klabu yake iliyompa jina zaidi Young Africans. Hii leo Jembe Fm inapata nafasi ya kuzungumza naye machache, suala kuu likiwa ni nini utofauti kati ya Yanga ya enzi zake na Yanga ya sasa?
HISTORIA YA SEKILOJO CHAMBUA KWA UFUPI
Akitokea Tukuyu Stars Jina lake lilianza kuwika zaidi wakati wa kombe la Chalenji (Afrika Mashariki na Kati) mwaka 1992, yeye akiwa na timu ya pili ya Tanzania Bara iliyoitwa "Kaka Kuona" (timu ya kwanza iliitwa Victoria) na kocha wake alikuwa Sunday Kayuni akisaidiwa na Charles Boniface. Kundi lao lilikuwa Arusha. Walifaulu kutinga nusu fainali wakakutana na Malawi, Waliifunga Malawi 1-0 kwa mkwaju wa penati. Chambua ndiye alifunga hilo goli Fainali ilikuwa chungu kwake na Taifa kwani "Kaka Kuona" walifungwa 0-1 dhidi ya Uganda. Kadhalika Chambuka alikuwa mchezaji tegemeo wakati Tanzania Bara wakinyakua ubingwa wa Chalenji ya mwaka 1994 iliyofanyika Kenya. Kikosi hicho chini ya Sylesaid Mziray na Sunday Kayuni kiliwafunga Uganda kwa changamoto ya mikwaju ya penati. Muunganiko wa Chambua, Lunyamila (Edibily) na Mohamed Hussein 'Mmachinga' iliwahi kuwa hatari kweli katika ligi kwa kufunga zaidi ya magoli 50 katika ligi.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.