Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Evarist Ndikiro. |
WADAU wa vyombo vya habari pamoja na Waandishi wa Habari hapa nchini wameombwa kulipa umuhimu wa pekee zoezi la Sensa ya watu na makazi litakaloanza Agosti 26 katika maeneo mbalimbali kote nchini.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkuu wa Mkoa wa Evarist Ndikiro alipokuwa akifungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali kutoka Wilaya zote na mikoa ya Kanda ya ziwa, Magharibi na kanda ya kati ili kutoa elimu tosha ya zoezi la uhesabuji sensa kwa jamii inayowazunguka.
Msikilize mkuu wa mkoa kwa kubofya hapa.
Amesema Vyombo vya Habari vinao umuhimu mkubwa sana katika kuuandaa umma na kuhamasisha Wananchi katika kulipokea zoezi hilo na hatimaye kufanikisha malengo yaliokusudiwa na Serikali katika kupata takwimu sahihi na kuweza kupanga mipango madhubuti ya maendeleo.
Ndikilo amesema kupitia Wahariri na Waandishi wa Habari katika vyombo mbalimbali wanayo nafasi kubwa ya kuwafanya Wananchi wakaelewa lengo la zoezi hilo ambalo Serikali imewekeza fedha nyingi ili kuhakikisha inapata takwimu sahihi ili kuweza kuharakisha maendeleo yanayokusudiwa kwa Wananchi wake.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza ameongeza kuwa Sensa ya mwaka huu inaumuhimu wake ili kuweza kufanikisha malengo ya melenia hivyo licha ya vyombo vya Habari pekee kufanya kazi za uhamasisha Taasisi nyingine zikwemo za dini,za Serikali na zile zisizo za Serikali zinapaswa kutoa ushirikiano ili kuweza kufanikisha zaidi.
Wanahabari wa vyombo mbalimbali kutoka kulia ni Paschal Michael, Shomari Binda, Juma Ntono na mdau kutoka Radio Ekwizera |
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Mwanza amewataka Wananchi kutoa ushirikiano kwa makarani na wasimamizi katika muda wote wa zoezi hilo litapokuwa linaendelea na kuongeza kuwa tayari wamekwisha kuziagiza kamati za ulinzi katika ngazi zote kuhakikisha kunakuwa na ulinzi kwa Wananchi na vifaa vyote vitakavyohusika katika zoezi hilo.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mkoa wa Mwanza. |
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.