Yanga |
Azam Fc |
Na Prince
Akbar
BAO pekee la
mwanasoka bora wa Uganda, Hamisi Kiiza ‘Diego’ dakika ya 110, jioni hii limeipa
Yanga tiketi ya kucheza Fainali ya Klabu Bingwa ya soka Afrika Mashariki na
Kati, Kombe la Kagame kwa mara ya pili mfululizo, na sasa itamenyana na Azam FC
keshokutwa, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiiza
alifunga bao hilo, kwa kichwa akiunganisha krosi ya karibu ya Haruna Niyonzima
ambaye alitumia mwanya wa mabeki wa APR kuzubaa wakisikilizia maamuzi ya refa,
baada ya Kiiza kuangushwa.
Yanga
waliinuka na wakaanzisha shambulizi la haraka lililozaa bao hilo. Dakika tatu
baada ya bao hilo, beki wa Yanga, Godfrey Taita alitolewa nje kwa kadi nyekundu
ya moja kwa moja na sasa ataikosa fainali.
Ikumbukwe
mwaka jana, Yanga iliifunga Simba SC katika fainali bao 1-0 na kutwaa taji la
nne la michuano hiyo, baada ya awali kutwaa Kombe hilo 1975, 1993 na 1999.
Mapema
katika Nusu Fainali ya Kwanza, Azam FC iliitoa AS Vita kwa kuifunga mabao 2-1,
mabao yake yakifungwa na John Bocco ‘Adebayor’ na Mrisho Ngassa, wakati la Vita
ya DRC lilifungwa na Mfongang Alfred.
Yanga SC;
Ally Mustafa ‘Barthez’, Juma Abdul/Shamte Ally/Juma Seif, Oscar Joshua,
Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Kevin Yondan, Athumani Iddi ‘Chuji’, Godfrey Taita,
Haruna Niyonzoma, Said Bahanuzi, Hamisi Kiiza na David Luhende.
APR; Jean
Ndoli Claude, Olivier Karekezi, Suleiman Ndikumana, Mugiraneza Jean, Johnson
Bogoole, Lonel St Preus, Ngabo Albert, Iranzi Jean Claude, Mbuyu Twite, Dan
Wagaluka na Tuyizere Donatien.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.