Dar
es Salaam. 'Bilionea' wa nyumba za Lugumi, Dk Louis Shika ameachiwa na
kwenda kupanda daladala kuelekea nyumbani huku akisema mpango wake wa
kununua nyumba za Lugumi uko palepale.
Baada ya kuachiwa na polisi leo
Jumanne jioni amesema kwamba bado mpango wake wa kununua nyumba hizo uko
palepale.
Amesema anachosubiri sasa ni fedha kuingizwa kwenye akaunti
yake na kulipa asilimia 25 anayodaiwa. "Siku nikipeleka fedha nataka
Yono na TRA waite waandishi wa habari waone na wautangazie umma,"
amesema.
Amesema vyombo vya habari vimetoa taarifa zake lakini
vitaumbuka siku akienda kupeleka fedha hizo.
Ameendelea kusisitiza
kwamba nyumba hizo zinahitajiwa na kampuni yake ambayo hakuitaja. Njiani
wakati akielekea kwenye kituo cha daladala cha Mnazi Mmoja, Dk Shika
alikuwa kivutio kwa watu aliokuwa akipishana nao.
Alipopanda daladala la
Tabata Mawenzi, kondakta alimkaribisha kwa kumweleza karibu mzee Shika.
Kauli hiyo iliwaamsha abiria ambao walikuwa na hamu ya kumwona. Dk
Shika alipanda daladala na kusimama huku akionyesha tabasamu lisiloisha.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.