Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akielezea tatizo la mfanyabiashara wa nyama ambaye amekuwa akipigwa na wafanyabiashara wenzake. |
Baadhi ya madiwani wakiwa kwenye kikao hicho. |
Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akisisitiza wafanyabiashara kutokubuguziwa na mtu yoyote kwenye shughuli zao wakati wa kikao hicho cha baraza. |
Diwani wa kata ya Kalangalala,Sospeter Mahushi akichangia swala la wafanyabiashara. |
Makamu Mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita pamoja na mkurugenzi wakijadili jambo wakati wa kikao cha baraza la madiwani. |
Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)wilaya ya Geita,Barnabas Mhoja Mapande akizungumza na madiwani wakati wa kikao hicho. |
Serikali
Wilayani Geita imesema kuwa mfanyabiashara anayehitaji kuwekeza kwenye
biashara ya kuuza nyama kwa bei nafuu anaruhusiwa kufanya biashara hiyo sawa na
watu wengine bila ya kubughudhiwa na mtu ama kikundi chochote.
Hatua hiyo
imekuja kutokana na mfanyabiashara ambaye jina lake halijafahamika mara moja
kufungua duka la nyama na kuuza kwa Sh,3500 kwa kilo kuambiwa na umoja wa
wamiliki wa maduka ya nyama kuwa afunge kwa kuwa wao wamekuwa wakiuza kwa Sh
6000 kwa kilo moja.
Amedaiwa
kuwa anauza nyama kwa bei ambayo haijazoeleka mjini Geita na kwamba bei hiyo
imezoeleka kwenye Kata ya Kasamwa .
Akizungumza
wakati wa baraza la madiwani wa halmashauri ya Mji wa Geita,Mwenyekiti wa
halmashauri ya hiyo Bw, Leornad Bugomola
alisema kumekuwa na kikundi kinachopanga bei ya nyama mjini humo na hivyo
kusababisha kumtoa mwekezaji aliyekuwa akiuza nyama kwa bei ya chini.
“Mkuu wa
wilaya kutokana na watu kuhangaika kufuata
nyama Kasamwa sisi tulionelea tumuombe mtu aje afungue Bucha ambayo itakuwa na
Bei nafuu hivyo alikubali lakini kimezuka kikundi ambacho kimekuwa kikimpinga
muwekezaji huyu na kwamba afunge bucha yake kutokana na wao kutokuafiki bei
hiyo ili swala nimeona nikwambie ili uweze kulishughulikia”Alisema Bugomola
Kutokana na
maombi hayo mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi alisema katika wilaya
anayoiongoza anataka kitu bora na kwamba suala la bei haliwezi kuwafanya watu
kutowekeza kwenye wilaya yake na kama kuna watu wengine ambao wanauza bei nafuu
ya nyama ni vyema wakapatiwa maeneo ya biashara hiyo kwani hakuna mtu ambaye
anaweza kuingilia biashara ya mtu mwingine.
Baadhi ya
wakazi wa mjini Geita wamepongeza uamuzi huo wa serikali kwa kuwa wengi hawana
uwezo wa kumudu bei ya nyama ya sasa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.