Gladys Wanga amewapa ruksa polisi kumfyatulia risasi, iwe isiwe atasonga kuingia uwanjani kumpokea Raila.
Watu watatu wameuawa hii leo wakati jeshi la
polisi la Kenya lilipojaribu kutawanya waandamanaji waliokusanyika
kupokea msafara wa kiongozi wa upinzani, Raila Odinga aliyerejea nchini
mapema leo akitokea nje ya nchi.
Polisi
ya Kenya imetumia gesi ya kutoa machozi na kufyatua risasi angani dhidi
ya wafuasi wa Odinga waliokuwa katika barabara inayotoka Uwanja wa
Ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta wakielekea mjini kati jijini
Nairobi.
Waandamanaji
wawili wameuawa katika mapigano yaliyotokea baina yao na polisi
waliokuwa wakitaka kuzua waandamanaji hao kuingia katika maeneo ya
kibiashara mjini Nairobi.
Ripo zinasema magari kadhaa yameteketezwa kwa
moto katika ghasia na machafuko hayo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.