ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 16, 2017

BREAKING NEWS: WATU WA 3 WAMEKUFA MAJI NA WENGINE 15 WAKIOKOLEWA BAADA YA MELI KUZAMA ZIWA VICTORIA

Watu 3 wamepoteza maisha na wengine 15 wakinusurika baada ya Meli ya Mv Julius kuzama ndani ya ziwa Victoria.

Meli hiyo inayo fanya safari zake Mwanza - Gozba imezama usiku wa kuamkia leo ambapo ilitarajiwa kuingia leo saa 12 asubuhi nazo taarifa za awali zinasema kuwa Chanzo cha ajali hiyo ni meli hiyo ni kutokea hitilafu kwenye injini yake sanjari na meli hiyo kuzidisha mzigo.

Zaidi ya magunia 500 ya dagaa yamezama na meli hiyo umbali wa kilometa 4 kutoka bandari ya Gozba.

Mwandishi wetu Zephania Mandia anafunguka kilichotokea kupitia kipindicha KAZI NA NGOMA kinachorushwa na Jembe Fm Mwanza (BOFYA PLAY KUSIKILIZA)... aa

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.