ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, October 29, 2011

MAHAKAMA YA KIMATAIFA YAWASILIANA NA MTOTO WA GADDAFI.

Wendesha mashtaka wa kimataifa wamekuwa na "mawasiliano yasiyo rasmi" na mtoto wa kiongozi wa zamani wa Libya Muammar Gaddafi. Mahakama ya uhalifu ya Kimataifa (ICC) imesema watu wa kati wametumika katika mazungumzo hayo yasiyo rasmi na Saif al-Islam.

Waendesha mashtaka wamesema mahakama imeweka wazi kwa mtoto huyo wa Gaddafi, kuwa anatakiwa kwa makosa ya uhalifu dhidi ya ubinadamu, na kuwa hana hatia hadi itakapo thibitishwa mahakamani.

Washirika
Saif al-Islam, ambaye alidhaniwa kuwa huenda angerithi utawala wa baba yake, amekuwa akijificha kwa miezi kadhaa.

Taarifa za hivi karibuni zinadai kuwa alikuwa kwenye msafara unaoelekea kwenye Jangwa la Libya karibu na mpaka na Niger, nchi ambayo washirika wengine wa Gaddafi wamekimbilia.

Lakini taarifa hizo hazijathibitishwa, na ICC imesema haifahamu yuko wapi.

Ofisi ya mwendesha mashtaka imeweka wazi kuwa iwapo atajisalimisha kwa ICC, atakuwa na haki ya kesi yake kusikilizwa mahakamani, na hana hatia hadi itakapothibitishwa.

Chanzo: bbc swahili

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.