ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 26, 2011

MTOTO WA MIAKA SITA AUNGUZWA VIGANJA NA MAMA YAKE MZAZI KISA SHILINGI 300

Idadi kubwa ya watoto wa mitaani mkoani Mwanza itazidi kuongezeka iwapo jamii haitobadilika katika suala zima la malezi bora yanayozingatia haki na usawa.

Hayo yamebainishwa leo jijini mwanza na Mkurugenzi wa kituo cha Farijika bi Asha Mtumwa pale mwandishi wa blogu hii alipotembelea kituo chake kinacho jihusisha na kutetea haki za watoto na wazazi cha Farijika Parents and Children Organisation cha jijini Mwanza na kukutana na mtoto Majaliwa Hassani (6) aliyeunguzwa vibaya viganja vya mikono yake na mamayake mzazi kwa kosa la kuiba kiasi cha fedha shilingi mia tatu.

Mtoto Majaliwa Hassani mwenye umri wa miaka sita viganja vyake hasa mkono wa kulia vimevimba, vimejaa maji kutokana na kuunuzwa katika jiko la mkaa, mtendaji wa unyanyasaji huo akitajwa kuwa ni mama yake mzazi.

Mara baada ya mtoto huyo kukiri kuchukuwa shilingi mia tatu na kuzitumia mchana, usiku ulipo wadia mama yake alichukuwa viganja vya mtoto huyo na kuvitia kwenye makaa ya moto.

Kwa maelezo ya majirani jana majira ya saa mbili usiku walisikia sauti ya mtoto huyo akilia kwa machungu kwa muda mrefu bila msaada…… asubuhi walivamia kwenye nyumba hiyo kujua kilichajiri nakukuta hali hiyo kwa mototo huyo huku mama akiwa ametoweka ndipo walipo amua kuchukuwa jukumu la kumpeleka kituo cha haki kwaajili ya kutafuta msaada zaidi.


Kituo hiki kisichokuwa na uwezo wa kifedha tangu Januari mpaka leo ni zaidi ya watoto 60 wamefikishwa kituoni hapo kuomba msaada wakiripotiwa kukutana na manyanyaso toka familia wanazoishi.

Mtoto Majaliwa akijieleza japo kwa shida.

Mtoto aliyeunguzwa Majaliwa Hassani(aliyelala) na kaka yake Maulid Hassani(8), watoto hawa hawaendi shule, mama yao ambaye ni mfanyabiashara wa mbogamboga sambamba na kupita majumba mbalimbali akifanya kazi ya kufua nguo huwaachia dagaa na unga wajipikie wenyewe.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.