Habari ambazo hazijathibitishwa inasema kuwa idadi ya waliokufa inaweza kuwa zaidi ya watu ishirini.
Imeelezwa kwamba idadi ya abiria walioondoka na basi hilo kutoka katika kituo kikuu cha mabasi ya mikoani Ubungo jijini Dar es salaam walikuwa arobaini na mbili lakini basi hilo linauwezo wakubeba abiria sitini na tano.
Hata hivyo msemaji wa hospitali ya Tumbi mkoani Kibaha Rose Mtei amesema kuwa mpaka jioni hii wamepokea majeruhi thelethini na tano wa ajali hiyo ambapo kumi na tatu wameruhusiwa, wengine wakiendelea kupatiwa matibabu zaidi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.