Jestina George ameshinda tuzo muhimu ya Blog ya Mwaka katika tuzo za BEFFTA zilizizofanyika Jumamosi tarehe 22 Octoba 2011 ndani ya ukumbi wa Lighthouse, Camberwell jijini London. Vazi lake lilibuniwa na KIKI wa Kiki's Fashion Tanzania.
Jestina akiwa na mdogo wake Luiza baada ya kupokea tuzo
Jestina Akila Pozi na wadau waliokuja kushoo Love
Jestina akiwa na marafiki zake waliokwenda kumsupport kutoka kushoto Jacque Maina, Jestina George, See Li, Amina Mussa & Zulfa Mussa
Frank Eyembe kutoka Urban Pulse, Lynn Kapinga, Jestina George, Mashel & Musa Sissasi Sarr.
Wakati akitoa Hotuba yake Jestina alianza kwa kumshuru Mungu ambae amemwezesha kumpatia uzima, afya njema pamoja na mafanikio makubwa aliyopata mwaka huu. Aliendelea kwa kuwashukuru Wazazi wake na mwisho wadau wote ambao walimpigia kura Pia Mabloggers na Tovuti mbalimbali ambazo zimemsaidia kumpigia debe na kuibuka mshindi wa BLOG OF THE YEAR 2011 kutoka kwenye kundi lenye Blog 15 za kimataifa. Hii ikiwa ni mara ya kwanza kwa Mtanzania kuingia, kushinda na kumfanya kuwa Mtanzania wa Kwanza kupokea tuzo za BEFFTA kwa upande wa Blogs
Jestina George ameitoa wakfu Tuzo yake kwa dada yake mpendwa Kissa George ambaye hatunaye tena hapa Duniani.
Maliza Wikendi Kibabe na Meridianbet
-
KAMA kawaida ni siku nyingine kabisa ya Jumapili ya wewe mteja wa
Meridianbet kuondoka na kitita cha mpunga. Mechi nyingi zitakuwa uwanjani
leo kusaka...
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.