
BONDIA Machachari nchini Mada Maugo amesema kuwa atamchapa kipigo cha mbwa mwitu bondia mwenzake kutoka nchini Kenya, Joseph Odhiambo kwenye shindano la raundi nane la ngumi linalotarajiwa kufanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba kesho(leo).
Aliyasema hayo jana muda mfupi mara baada ya kufanyika zoezi la kupimwa uzito kwa mabondia wote 12 watakaoshiriki katika pambano la leo.

Huku akionekana kujiamini akitumia kauli yake ya uzawa, Maugo alisema kuwa yuko bomba na amewataka watanzania na wapenzi wa ngumi hususani wale wa Kanda ya ziwa wajitokeze leo kwa wingi kuupata uhondo na kushuhudia jinsi ambavyo anamshikisha adabu jirani yake bondia kutoka nchini Kenya Joseph Odhiambo.

Naye Joseph Odhiambo kutoka nchini Kenya, licha ya kukiri kumfahamu Mada Maugo katika ulimwengu wa masumbwi na kuwashukuru wakazi wa mikoa ya kanda ya ziwa, alisema kuwa hana hofu juu ya pambano hilo kwa madai kuwa ametoka mbali na anaamini atashinda katika pambano hilo la raundi 8 kwa uzito wa kilo 72 (middle weight).

Jumla ya mabondia 12 watashiriki, ambapo pambano la utangulizi litakuwa ni kati ya mabondia maarufu nchini Rashid Matumla ambaye atacheza na Bondia kutoka mkoani Mara Emma Kichele katika uzito wa kg 79 light weight na Joseph Marwa atafungua dimba na bondia Irandi Chacha naye kutoka Musoma katika uzito wa kg 83 cruiser weight.
Kiingilio katika pambano hilo kitakuwa ni Sh. 5,000 jukwaa kuu, Sh. 3,000 mzunguko na Sh. 1,000 kwa watoto.


Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.