Jana baada ya hukumu alipoulizwa maoni yake kuhusu hukumu ya mahakama dhidi ya mashtaka aliyokabiliwa nayo Prof. Costa Mahalu aliwaomba waandishi wasome zaburi 17.
Zaburi 17 inasema:
1. Ee Bwana, usikie
haki, ukisikilize kilio changu, Utege sikio lako kwa maombi yangu, Yasiyotoka katika midomo ya
hila.
2. Hukumu yangu na itoke kwako, Macho yako na yatazame mambo ya
adili.
3. Umenijaribu moyo wangu, umenijilia usiku, Umenihakikisha usione
neno; Nimenuia kinywa changu kisikose,
4. Mintarafu matendo ya wanadamu; Kwa neno la
midomo yako Nimejiepusha na njia
za wenye jeuri.
5. Nyayo zangu zimeshikamana na njia zako, Hatua zangu
hazikuondoshwa.
6 Ee Mungu, nimekuita kwa maana utaitika, Utege
sikio lako ulisikie neno langu.
7. Dhihirisha fadhili zako za ajabu Wewe uwa okoae
wanaokukimbilia; Kwa mkono wako wa kuume, Uwaokoe nao wanaowaondokea.
8. Unilinde kama mboni ya jicho, Unifiche chini ya uvuli wa mbawa zako;
9. Wasinione wasio haki wanaonionea, Adui za roho
yangu wanaonizunguka.
10. Wameukaza moyo wako, Kwa vinywa vyao hutoa majivuno.
11. Sasa wametuzunguka hatua zetu, Na kuyakaza
macho yao watuangushe chini.
12. Kama mfano wa simba atakaye kurarua, Kama mwana-simba aoteaye katika
maoteo yake.
13. Ee Bwana, usimame, umkabili, umwinamishe, Kwa
upanga wako uniokoe nafsi na mtu mbaya.
14. Ee Bwana, kwa mkono wako uniokoe na watu, Watu wa dunia hii
ambao fungu lao li katika maisha haya. Matumbo
yao wayajaza kwa hazina yako, Hushiba wana,
huwaachia watoto wao
akiba zao,
15. Bali mimi nikutazame uso wako katika
haki, Niamkapo nishibishwe kwa sura yako.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.