KUPITIA MKUTANO MKUBWA WA DUNIA WA UCHUMI ULIOFANYIKA NA KUMALIZIKA LEO JIJINI DAR ES SALAAM HAKIKA TAIFA LETU LIMEFUNGUA UKURASA MPYA WA FURSA YA KIUCHUMI.
MKUTANO HUU WA 20 MAHUSUSI KWA BARA LA AFRIKA, ULIRATIBIWA NA JUKWAA LA UCHUMI DUNIANI LENYE MAKAO MAKUU HUKO GENEVA USWISI.
MKUTANO UMEFUNGUA MILANGO YA KIUCHUMI KWA TAIFA LETU, KUTOKANA NA UKWELI KWAMBA SASA TUMEINGIAKTK RAMANI YA UCHUMI WA DUNIA KWA KUFANYIKA MKUTANO HUU HAPA NCHINI KWANI KWA KIPINDI KIREFU MIKUTANO MINGI IMEKUWA IKIFANYIKA AFRIKA YA KUSINI KUTOKANA NA NCHI HIYO KUWA NA MIUNDOMBINU BORA ZAIDI YA KUHUDUMIA WAGENI WENGI KWA PAMOJA, KIGEZO AMBACHO TANZANIA IMEKITIMIZA HATIMAYE IKAWA MWENYEJI WA MKUTANO HUO ULOMALIZIKA KWA UFANISI.
ZAIDI YA WAGENI 1000 KUTOKA NCHI 85 WAKIWAMO WAKUU WA NCHI 11 WAMESHIRIKI MKUTANO HUU, DHAHIRI HALI IKIONESHA KUWA KUTOKANA NA MKUTANO HUU MIKUTANO MINGINE YA KIMATAIFA ITAKUWA IKIFANYIKA HAPA NCHINI KWANI WAGENI WANASIFA YETU NA UZOEFU WETU KTK KUFANIKISHA MIKUTANO MIKUBWA KAMA HUU ULIOISHA.
LENGO LA MKUTANO PAMOJA NA KUJADILI NA KUBADILISHANA UZOEFU WA KUJENGA UCHUMI NA KUIMARISHA UHUSIANO WA KATI YA MATAIFA YENYE UCHUMI MKUBWA NA YALE YA AFRIKA MAARUFU KAMA SOUTH - SOUTH CO - OP - ERATION.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.