ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, September 1, 2023

MWANADADA HUYU MLEMAVU ANATAMANI KUKUTANA NA RAIS SAMIA

 NA ALBERT G. SENGO/MWANZA

"Siri yangu ni Mwenyezi Mungu tu ndiye anayenipa moyo, ingawa mara nyingine nakata tamaa hasa pale bidhaa zangu zinaposhindwa kwenda sokoni kimauzo kwasababu soko ninalolitegemea ni mtandaoni na wateja kupata ni changamoto lakini sikati tamaa naendelea kutengeneza bidhaa nzuri za viwango" anasema mwanadada mjasiliamali Suki's Craft, Mtanzania mwenye asili ya Asia anayeishi jijini Mwanza akishiriki Maonesho ya Biashara ya Afrika Mashariki ya TCCIA yanayofanyika katika viwanja vya Furahisha kata ya Kirumba. Kisha akaongeza "Nimejiunga kwenye magroup mengi ya whatsaaap hivyo kila maonesho yakiitishwa naziona fursa za kushiriki" Jeh! nini ombi lake kwa Serikali na vipi siku akikutana na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan atamwambia nini? #jembefm #samiasuluhuhassan #ikulumawasiliano #tanzania #maoneshoyabiashara

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.