"WANANCHI MNARA UNASOMA 5G TU."
Mechi hii tofauti na ya KMC, JKT Tanzania waliwauliza Yanga Sc swali la utimamu wa mwili na Improvisation kutoka kwa wachezaji nyota wa Yanga.
Nidhamu ya kukaa nyuma na kuweka idadi kubwa ya wachezaji kuutazama mpira ilikuwa sahihi japo maswali makubwa kwao yalikuwa ni namna gani wataweza kushikilia bomba bila mpira kwa kuwa na nidhamu ile ile, concentrations ile ile, organization ile ile na ustahmilivu ule ule.
Bahati mbaya kwao Yanga Sc sio kuwa Bora tu Bali wana tanki la kutosha kucheza kwa spidi na intensity ile ile dakika 90 za mchezo.
Kocha Gamondi ana faida ya kujenga physique ya kutosha kwa idadi kubwa ya wachezaji wake kumnufaisha kutekeleza maelekezo yake kiwanjani.
Huyu Maxi Zengeli ukiachana na ubora wake sio na kificho ila ana Mentality ya kuutamani ushindi muda wote na inaisaidia timu.
5G haziji kwa hamasa ama bahati mbaya. (Maandalizi na ku settle dressing room kupata timu zaidi kuliko just star players )
CHUKUA HII TOKA KWANGU
Na KochaWaWhatsapp
Mwokoziwabunju
Niaminimimi
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.