ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, October 12, 2022

LANDESA:UWEKEZAJI WAJIBIFU WA ARDHI YA JAMII UTAPUNGUZA MIGOGORO

 

Mkurugenzi wa Landesa Tanzania, Godfrey Massay akipekua baadhi ya taarifa za ardhi wakati wa mafunzo ya wanahabari na wadau wa ardhi yaliyofanyika mjini Morogoro

Baadhi ya washiri wa warsha ya wanahabari na wadau wa ardhi.

Mtaalamu wa Ardhi wa Landesa, Masalu Luhula akichangia mada katika mafunzo ya wanahabari na wadau wa ardhi yaliyofanyika mkoani Morogoro

 

Na Tumaini Godwin, Morogoro

SHIRIKA la Kimataifa linalojihusisha na masuala ya Ardhi la Landesa limesema Uwekezaji Wajibifu wa ardhi ya jamii utasaidia kupunguza migogoro hasa baina ya wakulima na wawekezaji.


Akifungua mafunzo ya wanahabari na wadau wa sekta ya ardhi, Mkurugenzi wa Landesa Tanzania, Godfrey Massay  amesema ili uwekezaji uwe na tija lazima kuwe na uwajibikaji wa pande zote muhimu hasa Serikali, jamii na wawekezaji.  


Amesema moja ya masuala muhimu kwenye Uwekezaji Wajibifu ni ushirikishwaji wa makundi yote muhimu wakiwemo Wanawake, vijana na walemavu.


Kulingana na Massay, Landesa wameamua kuja na Kitabu cha Mwongozo wa Uwekezaji Wajibifu kwenye ardhi ya jamii kama dira ya kusaidia kufikia malengo ya uwekezaji huo


"Mwongozo huu ukitumika utasaidia kumaliza migogoro ya ardhi kwenye maeneo mengi," amesema Massay.


Afisa Ardhi wa Landesa, Masalu Luhula amesema zipo sababu nyingi zinazochangia kuwepo kwa migogoro ya ardhi baina ya wawekezaji na wananchi hasa vijijini.


Ameeleza kuwa miongoni mwa hizo nu uelewa mdogo kuhusu masuala ya ardhi kwa baadhi ya wananchi na ushirikishwaji hafifu.


Kwa upande wao baadhi ya wananchi wameomba kuendelea kupewa elimu kuhusu masuala ya ardhi.


"Wanakuja wawekezaji mnaongea kiswahili halafu wanaleta mikataba ya kingereza, ukisaini tu basi mnajikuta kwenye mgogoro. Kumbe ulisaini kitu hukielewi," amesema

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.