Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana akizungumza wakati wa siku hiyo
Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo akizungumza wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.
MRATIBU wa Watoto Jiji la Tanga Mwajuma Mustapha akizungumza wakati wa maadhimisho hayio
Wanafunzi wakiwa kwenye maadhimisho hayo
Na Oscar Assenga,TANGA.
MWAKILISHI wa Shirika la BRAC Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo amesema kwamba wao wamejikita katika harakati za kuwasaidia watoto wa kike kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazowakabili kwa utekelezaji wa mradi wa elimu kwa mkoa wa Tanga ili kuwawezesha waliokosa fursa hiyo kunufaika nayo.
Katika mradi huo wa elimu Shirika hilo limekuwa likitoa fursa za elimu ya awali yaani ECD kwa watoto wadogo ikiwemo watoto wa kike na elimu ya Sekondari kwa mabinti walio nje ya mfumo rasmi wa elimu kwa kutumia programu ilioharakishwa Accelerated Learning Program (QT).
Hayo yalibainishwa na Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Isihaka Mirambo wakati wa siku ya kilele cha mtoto wa kike duniani iliyofanyika kwenye viwanja vya Urithi Jijini Tanga.
Isihaka ambaye ni Msimamizi wa Miradi ya Elimu wa Shirika la Brac Maendeleo Tanzania Mkoani Tanga alisema kwamba katika utekelezaji wa mradi huo wameweza kuwafikia mabinti wengi ambao wamenufaika kupitia miradi yao.
Alisema kwa upande wa wanufaika wa shule za Sekondari mabinti 926 ambao wengine wapo katika ngazi tofauti tofauti kama vile wasichana 10 wapo vyuo vikuu mbalimbali nchini, wasichana 51 wapo kidato cha sita ,wasichana 25 wamehitimu katika vyuo vya kati mbalimbali nchini na wengine wapo katika ngazi ya Sekondari katika shule huria mbalimbali hapa Tanga.
Alisema pia wanufaika takribani 1376 wamepatiwa mafunzo mbalimbali yahusuyo elimu ya Afya ya Uzazi, Athari zitokanazo na matumizi ya dawa za kulevya, Ujasiriamali nk ikiwemo kuwawezesha vifaa kwa ajili ya kuanza shughuli za uzalishaji katika Jamii kwa lengo la kujiongezea kipato katika nyanja walizosomea kama vile ushonaji, utengenezaji wa batiki, sabuni na mapishi.
"Lakini pia watoto takribani 2100 tumewapatia elimu ya awali katika vituo vyetu vya malezi na makuzi vilivyopo katika shule za Serikali za Msingi Mkoani Tanga huku watoto wengine 772 wanaendelea kunufaika na elimu hiyo nchini ya Ufadhili wa NORAD na Brac Maendeleo ikiwa ni utekelezaji wa mradi huu "Alisema.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho ya siku ya mtoto wa kike duniani Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Dkt Sipora Liana alitoa wito kwa watoto wa kike wasikubali kurubuniwa.
Dkt Sipora alisema kwamba Rais Samia Suluhu amewajali sana watoto wa kike ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa madarasa bilioni 580 kwa ajili ya madarasa 29 na mwaka jana alitoa Bilioni 1.8 zaidi ya hapo alitoa Bilioni 2 ya madarasa.
Alisema pia Rais Samia alitoa fedha nyengine zaidi ya Bilioni 700 kwa ajili ya watoto wa kike timiza malengo kila mtoto 250,000 kwa ajili ya kuanzisha miradi ili kuepukana na vishawishike watoto wa kike waliopo mitaani .
"Lakini pia bado kwenye mapato ya ndani Rais Samia ametoa asilimia 10 ya mapato inaenda kwa vijana,wanawake na watu wenye ulemavu huko ndani wengi ni wanawake watoto wa kike"Alisema.
Awali akizungumza wakati wa maadhimisho hayo Naibu Meya wa Jiji la Tanga Mwanaidi Kombo bado watoto wa kike wana jukumu la kufanya ili kuondokana na adha ya kukosa maendeleo.
" Kama mlivyomsikia MC hapa amesema kwamba wapo watoto wenyewe wanawashawishi wajomba acheni tabia na tambueni jukumu lenu la kuleta maendeleo endelevu" Alisema
Naibu Meya huyo alitoa wito kwa watoto wa kike kuhakikisha wanasoma kwa bidii maana elimu pekee ndio inaweza kuwakomboa na watambue kwamba hakuna bahati ila waamini kwamba elimu ndio itawawezesha kuwakwamua .
Hata hivyo aliwatoa hofu watoto wa kike kwamba Serikali imeendelea kuuunga mkono juhudi za watoto wa kike kuhakikisha wananufaika na uwepo wa fursa mbalimbali zitakazo wawezesha kujikwamua kiuchumi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.