HALMASHAURI ya
Manispaa ya Iringa imepokea pesa kiasi cha Milioni 900 kutoka serikali kuu kwa
ajili ya ujenzi wa madarasa 45 ya shule za sekondari.
Akizungumza na
waandishi wa habari ofisini kwake Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Ibrahim Ngwada alisema kuwa Manispaa ya Iringa ilikuwa na uhitaji wa madarasa
56 ambayo yanatakiwa kujengwa katika shule za sekondari.
Ngwada alisema kuwa
serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imetoka pesa kwa ajili ya ujenzi wa
madarasa 45 hivyo wameisaidia Manispaa katika ujenzi wa madarasa hayo.
Alisema kuwa madarasa
11 yaliyobaki yatajengwa kwa kutumia mapato ya ndani kwa sababu serikali kuu
imewapunguzia mzigo wa ujenzi wa madarasa hayo.
Ngwada alisema kuwa
kiasi hicho cha pesa za ujenzi wa madarasa 45 itahusika katika shule kumi na
nne (14) zilizopo katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa.
Alisema kuwa shule
hizo kumi na nne (14) ni shule ya Sekondari Ipogolo madarasa 5,Kigungawe madarasa
3,Kihesa madarasa 4,Kleluu mazoezi madarasa 4,Kwakilosa Darasa 1,Lugalo darasa
1,Mawelewele madarasa 4,Mivinjeni Idunda madarasa 3,Mlamke Darasa 1,mlandege
madarasa 4, Mtwivila madarasa 5,Shabaha madarasa 3,Nduli madarasa 4 na
Tagamenda madarasa 3 ambapo kila darasa litaghalimu kiasi cha shilingi million
ishilini (20,000,000)
Meya Ngwada alisema kuwa pesa hizo zitaingia moja kwa moja kwenye akaunti za shule husika hivyo walimu na viongozi watakuwa wanazisimamia wanatakiwa kuwa makini na fedha hizo kwa ajili ya kuleta matokeo chanya yanayokusudiwa.
Ngwada alimazia kwa
kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu
Hassan kwa kutoa fedha hizo za ujenzi katika kukuza sekta ya elimu na
kuwaondolea usumbufu wazazi wa kuchangia ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa
45.
Aliwaomba wananchi wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa kumuunga mkono Rais kwa kazi kubwa anayoifanya kuleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania kwa ujumla wake.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.