Na Victor Masangu,Pwani
Maafisa Habari wa Halmashauri za Mkoani Pwani pamoja na Waandishi wa habari wametakiwa kuwa wazalendo na kutumia kalamu zao kwa weledi katika kuielimisha jamii juu ya umuhimu wa kuwapeleka watoto wao kujiunga katika vituo vya utayari kwa lengo la kupata fursa ya kujiunga na darasa la kwanza mwaka 2023.
Kauli hiyo imetolewa na Afisa habari wa Mkoa wa Pwani Zablon Bugingo wakati wa ufunguzi wa warsha ya siku moja ambayo imeandaliwa kwa lengo la kujadili mpango wa utayari ambao unalenga kuwasaidia watoto na kupata elimu ya awali kabla ya kujiunga na darasa la kwanza.
Bugingo alisema kwamba maafisa habari hao wanapaswa kuwa mstari ww mbele kwa kushirikiana na jamii nzima ya Mkoa wa Pwani kuwaelimisha kupitia mafunzo hayo waliyoyapata ili kuweza kufanikisha mpango huo wa utayari kwa watoto kujiandaa kwa ajili ya kuanza darasa la kwanza kwa mwaka ujao.
"Mpango huu ni vema ukaenda Sambamba na kuwaelimisha wazazi,walezi pamoja na jamii kwa ujumla hivyo maafisa habari wote ambao wameweza kupata fursa hii ya mafunzo sasa ni jukumu lao kutoa sapoti ya Hali na mali na ikiwemo kuandika habari hizi kwa wingi,"alisema Bugingo.
Kadhalika alibainisha kuwa watoto hao wanaandaliwa katika vituo hivyo vya utayari na wanapaswa kusoma kwa kipindi cha muda wa wiki 12 lengo ikiwa ni kuwandaa kupata uelewa juu ya mambo ya shule kabla ya kujikinga rasmi na elimu ya darasa la kwanza.
Baadhi ya washiriki wa Warsha hiyo akiwemo kaimu mkuu wa kitengo cha habari Wilaya ya Kisarawe Waziri Waziri ameahidi kuyatendea haki mafunzo hayo waliyoyapata kwa kuelimisha jamii juuu ya mpango huo wa utayari.
Naye Afisa habari wa Halmashauri ya Kibaha Innocent Byarugaba amesema kuanzishwa kwa mpango huo ni mkombozi mkubwa katika kuboresha sekta ya elimu kuanzia ngaziza chini ili kuwasaidi watoto hao kupata elimu ya awali na hatimaye kujiunga na dara
Naye Mwezeshaji wa Mafunzo hayo Hellen Kulwa amewataka Maafisa habari hao wa halmashauri kwenda kuzingatia Umri wa Watoto Ili Mwalimu asiache kazi ya kufundisha na kuanza kulea Watoto.
Mpango wa Shule Bora ni Program ya Serikali ya Tanzania ya Kuboresha Elimu ya awali na Msingi Kwa Ufadhili wa mfuko wa Ukaid wa Serikali ya Uingereza unatekelezwa Katika Mikoa Tisa ya Tanzania.
Katika warsha hiyo ya siku moja ambayo imeandaliwa na ofisi ya Elimu Mkoa wa Pwani imeshirikisha maafisa habari wa halmashauri zote,maafisa maendeleo ya jamii na maafisa ustawi wa jamii.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.