Wenyeji wa Kiambu wamekuwa wakishuhudi mitetemeko ya ardhi tangu Jumatatu.
Baadhi ya wenyeji wa Kaunti ya Kiambu wanaishi kwa hofu baada ya kushuhudia misururu ya mitetemeko ya ardhi katika eneo hilo, kwa siku mbili mfululizo.
Maeneo yaliyoathirika ni pamoja na mji wa Limuru na viunga vyake, Mutarakwa, Ngarariga, Manguo na Ngubi pamoja na maeneo ya Kikuyu kama vile Kerwa, Keroe na Nachu.
Wenyeji walisema mitetemeko hiyo ya ardhi ilishuhudiwa eneo hilo siku ya Jumatatu na Jumanne, na kudumu kwa muda sekunde kumi.
Tukio la kwanza liliripotiwa Jumatatu asubuhi mjini Limuru, kabla ya ingine kuripoti saa sita mchana na hatimaye usiku kabla ya maji kuzidi unga asubuhi.
Kwa mujibu wa taarifa iliyochapishwa na jarida la People Daily, Stanley Muturi anayeishi eneo la Manguo alisema kuwa mitetemeko hiyo ilishuhudiwa saa 10.20 usiku mnamo Jumatatu, kwa sekunde kadhaa.
Ushauri wa wataalam
Kwa mujibu wa afisa mkuu wa mazingira Kiambu David Kuria, serikali ya kaunti inashughulikia suala hilo la mitetemeko na kusaka maoni ya wataalam wa kutoka Chuo Kikuu cha Nairobi.
Alisema ripoti za awali kutoka kwa wanajiolojia zilifichua kuwa mitetemeko hiyo haikujiandikisha kwenye mfumo wa kukagua mitetemeko ya ardhi nchini. “Sitaki kusema mengi kuhusu suala hilo ila tunasubiri majibu kutoka kwa wataalama kabla ya kutoa taarifa tukiwa serikali ya kaunti,” afisa huyo alisema.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.