ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, July 17, 2019

KUMBE MAGUFULI ALIISHI IGOGO.......


UKIULIZA wakazi wa jiji la Mwanza ni wachae sasa wasiojua historia na sifa kuu ya maisha tata, iliyo tawala  kwa miaka mingi kwa watu wa viunga vya kata ya Igogo iliyopo wilaya ya Nyamagana mkoani hapa.

Matukio ya Wizi, Uporaji wa kutumia nguvu, Ubakaji na fununu za Ushirikina ni matendo yaliyotawala kwa kipindi kirefu hasa katika miaka ya nyuma, lakini wengi wanasema huwenda sababu kuu ya matukio hayo kushamiri ikawa ni kwa kuwa eneo hilo awali lilitambulika kama makazi ya watu wa hali ya chini ambao walikuwa wamechangamana na wachache wenye kipato kizuri hivyo suala la kuoneana wivu likapata nafasi.

Sawa tutazungumza sifa mbaya lakini pia IGOGO ina mazuri yake, kwanza inapatikana kwenye moja ya vilima vya miamba ya mawe viliyotawala eneo kubwa la ardhi ya Mwanza, mpaka ikaitwa ROCK CITY.

Pili IGOGO ndilo eneo lenye idadi kubwa ya uwekezaji wa viwanda vikubwa nayo reli ya kati inapita katikati ya IGOGO.

Lakini jingine kubwa usilolijua ni hili.... Hivi unajua Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alishawahi kuishi IGOGO? Msikilize yeye mwenyewe akifunguka hiyoo juzi Jumatatu ya tarehe 14 July 2019.

RAIS AFUKUWA KABURI JINGINE LA UPIGAJI FEDHA SERIKALINI.

"HATA  kuwapeleka wagonjwa nje kwenda kutibiwa ilikuwa DILI, ilikuwa ni FURSA kwa baadhi ya watendaji wa Serikali  wapo walikuwa wakipewa vibali kwa matibu ya nje kwa ugonjwa wa mafua ili mtu apate nafasi ya kwenda akiwa na akiambatana na msindikizaji  na wengine mpaka wanaenda na wake zao nayo Serikali inaingia gharama kwa wote" 

Ni moja ya makaburi ya upigaji yaliyofukuliwa JANA na Rais Magufuli wakati akifungua vitengo saba vya Huduma za tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando Mwanza akidai kuwa baadhi ya fedha katika mabilioni tunayodaiwa kwa waliokuwa wakienda kutibiwa nje ya nchi hayana UHALALI.

Kwa maana hiyo Rais amemwagiza Waziri wa Afya Ummy Mwalimu kwenda kufukua madeni na kuchunguza kama ni ya halali au laa, na kama si halali basi wadaiwa walioambatana na wagonjwa kwenda nje wakamatwe kuyalipa madeni hayo.........

Rais #JPM akiwa Hospitali ya Rufaa Bugando Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.