Daladala iliyogongwa na basi la Ally's. |
Ajali hizo zilitokea jana usiku katika barabara kuu ya Mwanza-Shinyanga katika maeneo ya Mitindo wilayani Misungwi na eneo la Buhongwa Dampo wilaya ya Nyamagana jijini Mwanza.
Ajali mbaya zaidi iliyosisimua na kusababisha vilio kuugubika mji wa Usagara wilayani Misungwi, ilitokea majira ya saa 1:40 Buhongwa, ambapo Basi la Allys lenye namba za usajiri T.691 AGP liligonga Daladala (Toyota Hiace)na kusabaisha vifo vya watu tisa ambao kati yao, saba walikufa palepale.
Mwonekano wa dalaldala kwa nyuma. |
Baadhi ya abiria waliokuwa katika ajali hiyo akiwemo Shija Francisco ambaye alijeruhiwa mkono wa kulia, basi hilo liliwagonga sehemu ya ubavu wa kulia na kusabisha Hiace hiyo ipinduke na kuviringika mara tatu nje ya barabara, wakati likijaribu kulipita roli moja lililokuwa mbele yake, kwenye kona.
“Ilikuwa ghafla mno tulipojikuta uso kwa uso na basi hilo ambalo halikuwa na taa, dereva akajaribu kulikwepa lakini hakufanikiwa, lilitugonga na kufanya gari letu lipinduke na kuviringika mara tatu.” Alieleza Franchisco mkazi wa Usagara huku akimlilia mkazi mwenzake Juma Basu (27) aliyekufa papo hapo.
Usiku huo wa ajali ilishuhudiwa miili ya watu hao ambayo baadhi ilikuwa imepondeka vibaya na kukatika viungo akiwemo mtoto wa miaka minne, Raphael Simon aliyekufa pamoja na baba yake Saimon Paschal(35), wakazi wa Usagara.
Kamanda Mulowola aliwataja wengine waliokufa katika ajali hiyo kuwa ni Eliakim Fredrick mkazi wa Igogo Mwanza, Stephen Mungisa (hatambulika makazi), Dismas Mpange (Usagara)na wanawake wengine wawili ndugu Shobo Lumecha na Gaudensia Lumecha, wakazi wa Geita.
“Abiria 15 walijeruhiwa katika ajali hiyo akiwemo dereva wa Hiace Anthony Maige (52) na kukimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando lakin dereva wa Basi la allys Elias Charles alikimbia tunamsaka.” Alieleza Kamanda huyo na kubainisha kuwa daladala hiyo ilikuwa imejaza watu kupita kiasi.
Basi la Ally's lililoigonga daladala na kusababisha vifo vya watu 9. |
Basi la Bunda Express lililomgona mwendesha baiskeli. |
Kamanda Mulowola amesema kuwa chanzo cha ajali hiyo ya basi la Bunda lililokuwa likitoka Dodoma kwenda Musoma, ni mwendo kasi na ametoa wito kwa madereva kuwa waangalifu na wazingatie sheria za usalama barabarani wanapotumia vyombo vya moto.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.