ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, September 14, 2010

SEPTEMBER 11, CHADEMA ILIPOTINGA MIRONGO MWANZA. YASEMA HIZI NI RASHA RASHA MVUA KAMILI YAJA...

MGOMBEA WA URAISI KWA TIKETI YA CHADEMA DR WILLIBROD SLAA AKIMTAMBULISHA BW. WENJE MGOMBEA WA UBUNGE KWA TIKETI YA CHAMA HICHO WILAYA YA NYAMAGANA, KIUFUPI ZILIIPUKA SHANGWE ZA KUTOSHA WAKATI MGOMBEA HUYU AKIOMBEWA KURA.

DK SLAA ALISEMA WATANZANIA WASIFIKIRI KUWA MADINI NA RASLIMALI NYINGINE ZITAKAA MILELE BALI ZINAPUNGUA KWA SABABU ZINAVUNWA NA HAZIZAI NA ANASHANGAA KUONA KUWA WILAYA KAMA GEITA YENYE UTAJIRI WA MADINI INAKOSA MAJI SAFI INGAWA NCHI INA MIAKA TAKRIBANI 50 YA UHURU.

KATIKA HATUA NYINGINE MWANASHERIA MAARUFU MABERE MARANDO AMEAHIDI KURUSHA MABOMU ZAIDI KUFICHUA ALIOUTAJA KUWA NI UOZO (SABABU ZA KUKWAMA KIUCHUMI)ILI KUIHAKIKISHIA CHADEMA USHINDI.

MGOMBEA URAISI WA TANZANIA KUPITIA CHADEMA DR WILLBROD SLAA AKIHUTUBIA MAELFU YA WAKAZI WA JIJI LA MWANZA KATIKA MFULULIZO WA KAMPENI ZAKE KWENYE UWANJA WA SHULE YA MSINGI MIRONGO.

WANANCHI WAKILA KIAPO KUKIHAKIKISHIA USHINDI CHAMA HICHO NGAZI ZA UDIWANI, UBUNGE HADI URAISI, MARA BAADA YA KUSOMEWA VIPENGELE VYA ILANI YA CHAMA HICHO.

ILANI YA CHAMA HICHO IMEGUSIA ELIMU, AJIRA, ULINZI NA USALAMA, KILIMO, AFYA, MICHEZO, NJIA ZA KUKUZA UCHUMI, RASLIMALI ZA TAIFA NA MENGINE MENGI.

NIKIRIPOTI KUTOKA JUKWAANI LA ZIADA LIPO ENDELEA KUCHUNGULIA BLOGU HII KUKUPA NEWz BIN NEWz KIPINDI HIKI TUKIELEKEA OCT 31.

Tupe maoni yako

7 comments:

  1. kaka ujumbe umefika, mwanza patachimbika nilikuwa sijapata picha kamili. JK halali kwa mtindo huu, masha aanze kufikiria utaratibu mwingine wa maisha

    ReplyDelete
  2. tumekuja wenyewe hatukuletwa na malori

    ReplyDelete
  3. Chadema oyeeeeee, tingatinga la kuung'oa ufisadi tanzania limekuja. Endelea kutumwagia data za kanda ya ziwa kaka gisengo.

    ReplyDelete
  4. Kaka nilikuwa ninaishi Mwanza -- mitaa ya Unguja well nimefurahi kuona umati wa watu wa Mwanza; Mwanza ni tajiri sana -- MAFISADI NJE MWAKA HUU

    KenRon --- Mmwanza aishie Marekani

    ReplyDelete
  5. JK aandae jembe akalime, Masha aanze kujikumbusha sheria arudie uwakili. Lakini wakumbuke kama walihusika kwenye ufisadi Dr. Slaa hatawaacha. Nchi imekombolewa huleeeeeeeeeee! mafisadi mwafaaaa.

    ReplyDelete
  6. Hapa ndo patamu kabisaaaaaaaa, mwaka huu wakiiba kura zetu watatujua sisi ni nani. Asante G. Sengo endelea kuuza blog usikosee kabisa unajua watumiaji wa net ni wasomi na wapinga ufisadi ni wasomi angalia hiki ndo kipindi cha kupata viewers wa kumwaga usikosee soma alama za nyakati

    ReplyDelete
  7. BLOG YA UKWELI. MASHA CHALI KAMA MENDE KUANGUSHA KABATI VILE. Jamaa alizidi pesa za migodi yote ya wilaya za Mwanza walikuwa wanakula na JK sasa mrija umekatika. Naomba wenje afichue yote afanye oditing'i na akamue hadharani. Si unacheki JK alivyokuwa ang'ang'ania Kifisadi chake kishinde walikuwa wanamtandao mkubwa. Nashukuru sasa mambo yatapungua yule mkurugenzi wa jiji la Mwanza bora afukuzwe kazi mwizi kinoma.. SHEN'ZAO sio tusi ni Kichina hicho.Buriani Masha Born 19.. DIED 2010.RIP

    ReplyDelete

Note: Only a member of this blog may post a comment.