ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 4, 2019

MAULID KITAIFA MWANZA YADHIHIRISHA KUWA TANZANIA NCHI PEKEE DUNIANI ISIYOTIKISWA NA UDINI.



 Pengine hili likawa mfano wa kuigwa duniani nalo linatokea katika nchi moja barani Afrika nayo ni Tanzania, nchi inayotajwa kuwa kisiwa cha amani, pale unapokuta viongozi wa dini kubwa ambazo zinapishana katika imani, zinashirikiana pamoja tena hatua kwa hatua kufanikisha sehemu ya mapokeo ya imani.

Ni katika ufunguzi wa maadhimisho ya wiki kuelekea sikukuu ya Mtume Muhammad ambapo maandalizi ya sherehe hizo zinafanyika kitaifa katika viwanja vya Furahisha jijini Mwanza yamefanywa na Kamati ya Amani inayoundwa na viongozi wa dini ya Kiislamu na Kikristo nao kwenye uzinduzi licha ya kutajwa waziwazi kama sehemu ya kamati vilevile viongozi hao wa dini ya Kikristo wametunukiwa zawadi kama kumbukumbu ya ushiriki wao.

Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa wiki ya Maulid ambayo maana yake ni "Mazazi" au Birthday kwa kiingereza..

Maulid ilianziashwa miaka 600 baada ya kifo cha Mtume (Swalla Allahu alayh wasalam) yaani karne 6 baada ya Mtume kuondoka duniani huko misri.
Watu wa kwanza kuanzisha kusherekea mazazi (Maulid) ya Mtume (Swalla Allaahu alayh wasalam) katika historia ya Uislam ni utawala wa Banu Ubaid ambao walijulikana kama Faatwimiyuun ambao ni Mashia waliokuwa wamejimegua kutoka kwenye kijikundi kingine cha shia (Ismailiya)
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa ufunguzi wa wiki ya Maulid akihutubia umma uliofika kwenye viwanja vya Furahisha vilivyopo katika kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini humo.
 Mjumbe wa Baraza la Ulamaa Sheikh Issa Othman Issa akitoa neno kumkaribisha mgeni rasmi. 
 Sheikh Mkuu mkoa wa Mwanza Hassan kabeke akifafanua jambo kwenye kusanyiko hilo la ufunguzi wa wiki ya Maulid katika viwanja vya Furahisha vilivyopo katika kata ya Kirumba wilayani Ilemela jijini humo.

 Meza kuu na umakini wake.
 Sehemu ya waumini waliojitokeza. 
 Pia kulikuwa na mabanda ya uelimishaji na utoaji mafunzo.
 Bidhaa mbalimbali za miongozo ya dini zitapatikana kwa kipindi chote cha maadhimisho.
 Inatokea Tanzania pekee.
 Kauli mbiu ya Maulid 2019.
 "Ndugu wakutanapo" mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella akifurahia jambo na aliyekuwa Mkuu wa wilaya ya Ilemela Mama Amina Masenza (kushoto) 
 Katika taarifa iliyotolewa miezi kadhaa iliyopita na Katibu Mkuu wa baraza hilo, Mohammed Khamis Said, kwa vyombo vya habari, iliainisha Maulid ya kitaifa kuadhimishwa usiku wa Jumamosi, mwezi 11 RABIUL AWWAL 1441H sawa na Novemba 9, 2019 katika viwanja vya Furahisha Jijini Mwanza na Baraza la Maulid litafanyika Jumapili Novemba 10, ambayo ndiyo itakuwa siku ya mapumziko kitaifa. 

Baraza litaanza saa 9:00 Alasiri katika ukumbi wa Benki Kuu (BOT), Kapripoint, Mwanza.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.