Njombe
Mahakama ya hakimu mkazi mfawidhi
wilaya ya Njombe imemhukumu kifungo cha maisha jela mtuhumiwa Addo Aron Nziku
baada ya kukutwa na hatia ya kubaka mwanafunzi mwenye umri wa miaka 8 katika
kijiji cha kitulila halmashauri ya mji Njombe.
Shauri namba 31 la mwaka 2019, ni
kesi iliyomkabili mtuhumiwa Addo Aron Nziku mwenye miaka 26 mbena na mkazi wa
kijiji cha matola halmashauri ya mji Njombe, dhidi ya jamhuri.
Shauri hili likiwa chini ya hakimu
James na Mhanusi na Mwendesha mashataka wa serikali Nura Manja ambae ameieleza
mahakama kuwa mtuhumiwa anadaiwa kumwingilia mwanafunzi huyo zaidi ya mara tatu
kabla ya mtoto huyo kumweleza bibi yake juu ya maswahibu yanayompata.
Mtuhumiwa Addo Nziku anadaiwa
kumwingilia kimwili mtoto huyo kwa zaidi ya mara tatu katika eneo la mabanzi
yaliyoko nyuma ya nyumba ya wazazi wa mtoto huyo huku mara ya tatu akimuingilia
katika eneo la kukata majani ya mifugo ambako mtoto huyo alitumwa kwenda kusaka
majani ya simbilisi siku ya tarehe 26 mwezi wa kwanza.
Mahakama imemtia hatiani mtuhumiwa
baada ya kujiridhisha na ushaidi uliotolewa kwa kumkuta na hatia ya kubaka
kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili
E sambamba na kifungu namba 131 kifungu kidogo cha tatu cha kanuni ya
adhabu namba 16 kama ilivyofanyiawa marejeo mwka 2002.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.