ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, November 9, 2019

RC MWANZA AFUNGUKA MKUTANO WA MARAFIKI WA HABARI.




Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella amefungua mkutano wa wasaa wa marafiki wa Habari mkoani Mwanza ulioandaliwa na Klabu ya Waandishi Habari Mkoa Mwanza (MPC).

Akifungua mkutano huo Novemba 09, 2019 jijini Mwanza, Mongella amesema Serikali inatambua mchango mkubwa wa vyombo vya habari hivyo itaendelea kushirikiana na wabahabari katika kuchochea maendeleo.

Aidha Mongella ameipongeza MPC kupitia Mwenyekiti wake Edwin Soko kwa kuandaa mkutano akisema utasaidia kujadili fursa mbalimbali mkoani Mwanza ikiwemo ukarabati na ujenzi meli mpya katika Ziwa Victoria pamoja na ujio wa reli ya kisasa (SGR) huku ukitoa picha halisi katika kuelekea kwenye mkutano mkubwa wa Jukwaa la Biashara mkoani Mwanza utakaofanyika mwaka ujao.

Naye Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko amesema mkutano huo unalenga kuimarisha ushirikiano baina ya vyombo vya habari na wadau katika kufanikisha ajenda ya maendeleo mkoani Mwanza huku akisisitiza wanahabari kufanya kazi kwa weledi ili kulinda mustakabali wa amani kwa Taifa.
Mkuu wa Mkoa Mwanza, John Mongella akizungumza kwenye ufunguzi wa mkutano huo.
Mwenyekiti wa MPC, Edwin Soko akitoa salami za ufunguzi kwenye mkutano huo.
Wanahabari na marafiki wa habari wakifuatilia mkutano huo.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.