Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.
Ofisi ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, sera, Bunge, Kazi, Ajira, Vijana na watu wenye ulemavu, imetoa hali ya dawa za kulevya hapa nchini kwa mwaka 2018, na kuiwakilisha kwa wabunge.
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dodoma, Waziri mwenye dhamana ya Ofisi hiyo, Mhe. Jenista Mhagama, amesema lengo la kutoa taarifa hiyo kwa jamii, ni kuwafahamisha wananchi hali ya dawa za kulevya hapa nchini na jitihada za serikali katika kupambana na tatizo hilo.
"Aidha taarifa hii imewasiishwa kwa wabunge ili waweze kuwaelezea wananchi kwenye majimbo yao Hali halisi ya tatizo la dawa za kulevya hapa nchini na jitihada zinazofanywa na serikali katika kupambana na tatizo hilo" amesema Waziri Jenista.
Amesema vyombo vya dola kwa kushirikiana na wananchi viliendelea kutekeleza agizo la Rais Dkt John Magufuli, katika kumuwezesha nchi yetu na kupata mafanikio katika kudhibiti dawa hizo, kwa mujibu wa Shirika la kimataifa la kupambana na dawa za kulevya(UNODC) Tanzania umepungua uingizaji nchini wa dawa za kulevya aina ya heroin kwa asilimia 90.
Ameongeza kuwa "licha ya jitihada hizo lakini bangi bado ni tatizo kubwa hapa nchini, na mikoa ambayo imeonekana kuathirika zaidi na kilimo cha bangi ni pamoja Mara, Tanga, Morogoro, Arusha,Kagera na ruvuma" amesema.
Pia milungi imeendelea kutumiwa na watu wa rika mbalimbali kwa kipindi cha mwaka 2018, juhudi za za vyombo vya dola vimefanikiwa ukamataji wa tani 24.3 za bangi na watuhumiwa 10,061, na tani nane 8.97 za mirungi na watuhumiwa 1,186.
Aidha amebainisha kuwa serikali imeendelea kutoa huduma za tiba kwa watumiaji wa dawa za kulevya na jumla ya vituo sita vilivyopo katika mikoa ya Dar es saalam, Mwanza, Mbeya na Dodoma viliendelea kupatiwa huduma za methadone.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.