ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 6, 2019

UJENZI WA CHELEZO KWAAJILI YA MELI MPYA ZIWA VICTORIA WAWASISIMUA MA-SHEIKH - WASHUSHA DUA KWA JPM


Wakati zoezi la kuandaa uso wa kazi tayari kwa kuanza ujenzi wa Chelezo kitakachotumika kujengea Meli mpya katika Ziwa Victoria likiendelea kwa kasi katika eneo la Bandari ya Mwanza Kusini, Ma-Sheikh na waumini wa dini ya Kiislamu kutoka ndani na nje ya nchi waliofurika jijini Mwanza kushiriki Maulid inayofanyika kitaifa mkoani hapa wanapata nafasi kutembelea kujionea uwekezaji huo.

Sheikh Mkuu wa mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke Baada ya kutembelea eneo hilo na kushuhudia hatua mbalimbali za uwekezaji wa ujenzi wa kisasa unaoendelea na kubadili kabisa taswira ya eneo la bandari, anaamua kuwasilisha mawazo na minong'ono iliyokuwa ikitawala kwenye vinywa vya waumini wenzake wakati wakiendelea na ziara na kuamua kuwasilisha hisia zao mbele ya Wandishi wa Habari.

"Wakati mwingine wakisema hawa (huku akimnyooshea kidole Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella) tunaweza kusema kuwa wanajitetea, lakini wakati mwingine tuseme sisi juu ya haya makubwa yanayofanywa na Serikali ya awamu ya Tano chini ya Rais Magufuli kwani tuna haki kama Watanzania" Alisema Sheikh Kabeke na kisha kuongeza "Nitoe wito kwa Watanzania wakipata fursa watembelee miradi hii ya Serikali ili iwatoe upofu"

"Sasa kwa heshima na taadhima tunamuweka kati Mkuu wa Mkoa Bwana Mongella amwakilishe Mhe. Rais John Pombe Joseph Magufuli, kwa niaba yake kuzipokea dua zetu Waislamu tuliofika hapa tukaona kwa jicho hili la nyama yale yanayofanywa na Serikali yake"

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.