Dkt. Adephonce Fuka, kutoka Chuo kikuu Huria akitoa mada kuhusu mwenendo wa Elimu ya Masafa kwa Madiwani katika Mkutano wa 34 wa Jumuiya ya Serikali za Mitaa ALAT jijini Dodoma.
Baadhi ya Madiwani wakiwa katika Mkutano huo wa 34 wa Jumuiya ya ALAT, huku wakitazama na kuona jinsi watakavyokuwa wakinufaika na Elimu ya Masafa kupitia Simu zao za Adroidi. (Picha na Habari na Atley Kuni wa OR TAMISEMI)
Elimu ya Msafa kuwajengea uwezo MadiwaniNa. Atley Kuni- OR TAMISEMIMadiwani kote nchini wataanza kupata mafunzo ya uongozi kwanjia ya masafa kupitia mtandao wa kielektroniki, yaani kupitiamfumo wa intaneti, hali itakayowawezesha kujiimarisha katikautendaji wa majukumu yao ya kila siku na kuwatumikia wananchi.
Akitoa mada katika mkutano mkuu wa 34 wa Jumuiya ya Serikaliza Mitaa nchini, Mhadhiri wa chuo Chuo Kikuu Huria, Dkt.Adephonce Fuka, alisema shabaha ya mafunzo hayo nikuwajengea uwezo Madiwani ambao ni wawakilishi wa wananchikatika maeneo yao.
Akizungumza wakati wa mawasilisho, Dkt. Fuka alisema nia kuu nikuhakikisha Madiwani wanatekeleza majukumu yao kwa mujibuwa sheria, taratibu na kanuni zinazoongoza mabaraza yamadiwani, na mafunzo hayo ni maboresho ya kitabu cha rejea yaMh. Diwani kilichotumika kufundisha Madiwani kutoka Mamlakaza Serikali za Mitaa 93 hapo awali.
Mafunzo hayo ambayo yameandaliwa kwa mtindo wa Elimu-Masafa ili kuwezesha kujifunza mahali popote, yataendeshwa naChuo cha Serikali za Mitaa - Hombolo, na ni marejeo ya mafunzoya awali ambayo yalitolewa kwa viongozi hao kwa Halmasahuri 93zilizopo chini ya mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta za Umma(PS3).
Akitoa maelezo ya awali kabla ya kutolewa kwa wasilisho la elimuhiyo ya masafa kwa njia ya kieletroniki, mwakilishi kutoka PS3,Dkt. Peter Kilima, alisema mradi huo unaofadhiliwa na Serikali yaMarekani kupitia Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani(USAID), unafanya kazi katika mikoa 13 na Halmashauri 93 natayari umejipanga kutoa elimu kwa madiwani nchi nzima.
“Mradi huu ni wa miaka mitano, na moja ya maeneotunayoimarisha ni mfumo ya Utawala Bora na Ushirikishwaji wa Mfumo wa Kielektroniki.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.