ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, September 29, 2018

BREAKING NEWS:- SIKU YA 9 MV NYERERE YASIMAMA WIMA ASILIMIA 100, WAMEKUTA NINI NDANI?



NA. GSENGOtV
UKARA

Siku tisa zinakamilika hii leo tangu taifa la Tanzania kupoteza zaidi ya watu 220 kwenye ajali ya kupinduka majini kwa kivuko cha #MvNyerere. Gari ya mizigo aina ya Canter tani 1 na nusu, Pikipiki 1 yenye namba za usajili DFPA 2313 na baiskeli ambayo bila shaka ilikuwa ya mkulima.

Vyote hivyo vimeokotwa ndani ya maji na wazamiaji maalum wakishirikiana na wazawa eneo lilelile la ajali. 

Katika hatua nyingine ya kufunga zoezi la upokeaji michango, Kamati ya Maafa iliyochini ya Mwenyekiti wake ambaye pia ni Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Issack Kamwelwe, hii leo kabla ya saa 7 mchana (muda wa kuhitimisha zoezi la uokoaji na upokeaji michango) imepokea mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi za kitanzania milioni 50 toka Kampuni ya Uzalishaji Umeme Tanzania (SONGAS)  pamoja na hundi nyingine ya mfano yenye thamani ya shilingi milioni 80 kutoka kwa ACACIA, fedha ambazo zote tayari zimeingizwa benki.

 Kwa sasa kivuko kiko wima kwa asilimia 100% pembezoni mwa ufukwe wa ziwa Victoria kijiji cha Bwisya, Ukara, wilayani Ukerewe mkoani Mwanza. 





Tangu walipoanza kazi hiyo asubuhi leo Septemba 29, 2018, wazamiaji tayari wameopoa pikipiki moja na baiskeli, jana walifanikiwa kutoa gari aina ya Toyota Canter.
Mikoba ya mikononi, mifuko yenye bidhaa za aina mbalimbali za viatu vya watu wazima na watoto ni miongoni mwa mali zinayoopolewa kutoka chini ya maji.
Vitu vingine vinatolewa katika kivuko hicho ambacho tayari kimevutwa hadi pwani ya mwalo la kijiji cha Bwisya kisiwa cha Ukara wilayani Ukerewe.
Kivuko cha Mv Nyerere kilipopinduka Septemba 20 na kusababisha vifo vya watu 230 huku watu 41 wakiokolewa.






Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.