ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 1, 2018

PICHA ZAIDI KUUNGUA KWA SOKO LA MLANGO MMOJA MWANZA.


NA. ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV
MWISHONI MWA WIKI  Ijumaa majira ya alfajiri September28,2018 Moto usiojulikana chanzo chake uliteketeza soko la Mlango Mmoja jijini Mwanza.


Licha ya jitihada za kudhibiti moto huo maduka na mabanda zaidi ya 500 ya wafanyabiashara yameteketea na mengine kadhaa kuungua upande mmoja.
Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella alikuwa mtu wa kwanza kufika eneo la tukio.
Akiwa sanjari na Mbunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula, Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ambaye pia ni Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella hatua kwa hatua akikagua kuungua kwa soko hilo.
 Hili nalo litapita.
Kamanda wa jeshi la polisi mkoani mwanza Jonathan Shanna tukioni katika ukaguzi.
 Mzingira toka eneo ambalo lilikuwa maarufu kwa mafundi vyereheni washoni wa nguo.
Ni kama kila mmoja anajiuliza ... Nini kifanyike, tunaanzia wapi?
 NA. ZEPHANIA MANDIA GSENGOtV
Vibanda 150 na maduka zaidi ya  100 katika soko la mlango mmoja lililopo kata ya mabatini jijini mwanza vimeteketea kwa moto ulizuka saa 11 alfajiri na kusababisha hasara kubwa ya thamani za bidhaa mbalimbali ikiwemo nguo.

Tukio la moto huo uliotekeza vibanda vya wafanyabiashara hao unadaiwa ni majiko ya mkaa ya baadhi ya mama ntilie waliuacha moto ukiwaka kwa ajili ya kuchemsha maharagwe.
 Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella,pamoja na kuwapa pole wafanya biashara wa soko hilo, ameagiza soko hilo lifungwe kwa muda wa siku mbili waka wakiendelea kuchunguza chanzo cha moto huo.

Aidha kamanda wa jeshi la polisi mkoani mwanza Jonathan Shanna,akiwa katika eneo hilo la soko la mlango,amesema wafanya biashara waendelee kuwa watulivu na kuwahakikishia usalama wakutosha katika eneo hilo.
 Wakati huo huo mbunge wa jimbo la nyamagana Stansilaus Mabula, amefika katika eneo hilo na kuwapa pole wafanyabiashara waliounguliwa na vibanda vyao,nakuwaomba kuwa watulivu katika kipindi hiki kigumu wakati serekali ikiendelea na kutafuta chanzo cha moto huo.
Wafanyabiashara wa mlango moja wameiomba serekali wanapojenga maeneo ya soko,kuangalia miundo mbinu ya magari ili kuondoa changamoto yanapotokea majanga ya moto.  

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.